Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametekeleza mambo manane mapya ambayo hayakuwamo kwenye orodha ya ahadi zake za mwaka jan...
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametekeleza mambo manane mapya ambayo hayakuwamo kwenye orodha ya ahadi zake za mwaka jana wakati alipoingia madarakani.
Siku chache baada ya kuapishwa, Makonda alikutana na wenyeviti wa Serikali za mtaa na kuwaeleza mikakati tisa aliyopania kuifanya katika kulibadilisha Jiji la Dar es Salaam.
Jumatano iliyopita, Makonda aliadhimisha mwaka wake mmoja tangu ateuliwe kushika wadhifa huo akielezea mambo 10 aliyoyafanya katika kipindi hicho na mengine 10 atakayoyafanya katika mwaka wake wa pili.
Wachambuzi wa masuala ya sayansi ya siasa wamempongeza kiongozi huyo na kusema hata kama hajatimiza baadhi ya ahadi, lakini amekuwa mbunifu kwa kujifanyia tathmini ukilinganisha na viongozi wengine.
Mipango aliyotekeleza
Mambo aliyotekeleza ambayo hayakuwamo kwenye orodha ya mikakati yake ni kampeni ya mti wangu, ujenzi wa wodi ya wagonjwa, vita ya dawa za kulevya, ujenzi wa ofisi ya Bakwata, kampeni ya uchangiaji wa damu, marufuku ya shisha na migogoro ya ardhi.
Kwa ufupi
Siku chache baada ya kuapishwa, Makonda alikutana na wenyeviti wa Serikali za mtaa na kuwaeleza mikakati tisa aliyopania kuifanya katika kulibadilisha Jiji la Dar es Salaam.



