http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Muungano wa Madaktari wa Kenya (KMPDU), wawakataa Madaktari wa Tanzania

Umoja wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umep...


Umoja wa Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Meno nchini Kenya ‘Kenya Medical Practitioners, Pharmacists and Dentists’ Union’ (KMPDU) umepinga vikali hatua ya Serikali ya Kenya kuleta madaktari kutoka Tanzania wakati Kenya ina madaktari wengi ambao hawaajiriwa.


Kupitia kwa Katibu Mkuu wa KMPDU, Ouma Oluga umepinga hatua hiyo na kudai kuwa Serikali ya Kenya haijawa makini katika kushughulika na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo.


Akizungumza na mtandao wa The Star wa nchini Kenya siku ya Jumamosi, Oluga alisema hata hivyo watawakaribisha madaktari kutoka Tanzania na kuwaunganisha katika umoja huo na kwamba watapaswa kupitia mitihani itakayoandaliwa na bodi ya wauguzi.


Amesema mitihani hiyo itachukua sio chini ya miezi mitatu labda kama tu hitaji hilo halitaangaliwa.


“Kenya ina zaidi ya madaktari 1,400 ambao wanasubiria ajira. Itakuwa gharama kubwa na dalili ya kushindwa kutumia fedha za umma vizuri kwa kuwa na madaktari 500 wa kitanzania kwa gharama ya Shilingi 20,000 kwa siku,” amesema.


Oluga amesema kuwa Kenya inapaswa kupitia upya utaratibu wake wa Rasilimali Watu kwa mujibu wa miongozo ya Afya kama ambavyo KMPDU imekuwa ikihitaji hapo kabla.


“Hatuwezi kuwa tunafanyia majaribio maisha ya wakenya katika hali inayoonesha kutowajali wananchi,” ameongeza.


Mapema jana Rais Magufuli alikubali na kuridhia ombi la Serikali ya Kenya na kuahidi kutuma madaktari 500 kusaidia kukabiliana na tatizo la upungufu wa madaktari nchini humo kufuatia mgomo wa madaktari ulioisha hivi karibuni baada ya kudumu kwa siku 100.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Muungano wa Madaktari wa Kenya (KMPDU), wawakataa Madaktari wa Tanzania
Muungano wa Madaktari wa Kenya (KMPDU), wawakataa Madaktari wa Tanzania
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiAyTHbZZxj2LUh9MXSCvxPy37InJrL3oquOGegrvr00nQ97tRFU6bAVQgler0kC3sxAj9iyOlPf1UDOZkfw36cxbHrh5v13MikCv28Ij4tKytNtbdPY1mIqBsRwi7Q7aAhiXT9_olgArN/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjiAyTHbZZxj2LUh9MXSCvxPy37InJrL3oquOGegrvr00nQ97tRFU6bAVQgler0kC3sxAj9iyOlPf1UDOZkfw36cxbHrh5v13MikCv28Ij4tKytNtbdPY1mIqBsRwi7Q7aAhiXT9_olgArN/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/muungano-wa-madaktari-wa-kenya-kmpdu.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/muungano-wa-madaktari-wa-kenya-kmpdu.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy