“we mzuri,we mkari kama Wema,sio kiburi sio mchafu ka Si Wema“,huo ni mstari mmojawapo unaopatikana kwenye wimbo mpya wa Dogo Janja,Kideb...
“we mzuri,we mkari kama Wema,sio kiburi sio mchafu ka Si Wema“,huo ni mstari mmojawapo unaopatikana kwenye wimbo mpya wa Dogo Janja,Kidebe ambapo inaaminika amelenga kumponda aliyekuwa mpenzi wa Nay wa Mitego anayefahamika kama Si Wema.
Alipoulizwa kuhusu mstari huo,Dogo Janja alidai kuwa yeye hajamaanisha kumponda wala kumchafua Si Wema ambaye watu wanamjua kama mpenzi wa zamani wa Nay wa Mitego bali kuna mwanamke mtaani kwao anaitwa Si Wema ana tabia chafu.
“kwa watu watu wanaodhani nimemaanisha Si Wema wa Nay wa Mitego,sio kweli.Mtaani kwetu pale kuna dada anaitwa Si Wema,pale Ngarenaro,sio mchoyo,Si Wema wa Ngarenaro sio wa Nay.” alisema Dogo Janja.