Rapa Rick Ross amemsajili msanii mpya kwenye lebo yake ya Maybach Music Group. Msanii huyu ni kijana asiyekuwa na makazi na alikutana na...
Rapa Rick Ross amemsajili msanii mpya kwenye lebo yake ya Maybach Music Group. Msanii huyu ni kijana asiyekuwa na makazi na alikutana na rapa Rick Ross barabarani na kijana huyo alianza kuchana mbele ya The Boss ilikupata nafasi ya kuwa kwenye lebo yake.
Isa Muhammad,ni rapa asiyekuwa na pahali pakuishi na kwao ni California ametangazwa kuwa msanii mpya wa MMG.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari RickRoss anasema hakutegemea kumsaini msanii huyu ila uwezo na moyo wake umemfanya awe rahisi kumkubali.
Rais wa MMG Kendall “Young Sav” Freeman amesema “Rick Ross ameona kitu kizuri kwenye maisha ya mbele ya Isa Muhammad,kipaje chake ni original”