Msanii wa bongo fleva Barakah da Prince ametaja mafanikio aliyoyapata kwa muda mch...
Staa huyo anayetamba na kibao cha siwezi amesema kuwa kwa muda mchache toka ameingia mkataba na label hiyo ameweza kufanya media tour nje ya Tanzania yaani Kenya,pia amefanya colabo nyingi na wasanii wa Kenya na Nigeria na pia amefanya video na director mkubwa ambaye hakutamja ila alidai ameshafanya kazi na wasanii wakubwa kama WizKid na Davido.
” Kwa mara ya kwanza nimeweza kufanya media tour nje ya Tanzania,nimefanya media tour karibuni kwenye radio na TV zote za Kenya na baadhi ya magazine,kuna colabo nimefanya na wasanii wa Kenya pia Nigeria ambazo siwezi kuzingumzia zaidi kwa sasa,Rock Star ni watu ambao anaamini wataijenga brand yangu na kifikisha ile sehemu nataka” Baraka da Prince aliiambia Dj Show ya radio One
Source: Radio One