Msanii mpya wa muziki ‘Mimi Mars’ kutoka label ya Mdee Music ya muimbaji Vanessa Mdee amezindua video yake mpya ya wimbo Sugar. Uzindu...
Msanii mpya wa muziki ‘Mimi Mars’ kutoka label ya Mdee Music ya muimbaji Vanessa Mdee amezindua video yake mpya ya wimbo Sugar.
Uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa na mastaa mbalimbali wa muziki, umefanyika Ijumaa hii katika Club ya Next Door Masaki jijini Dar es salaam.
Akiongea na Bongo5 wakati wa uzinduzi huyo, Mimi Mars amedai wimbo huo utamtambulisha ramsi kwenye game ya muziki.
“Wimbo unaitwa Sugar na kwanini Sugar ni kwa sababu ukijua mapenzi ni kitu kizuri, mapenzi ni matamu, kwa hiyo ni kama Sukari Sugar,” alisema Mars.
Muimbaji huyo alisema anaishukuru label ya Mdee Music kwa kuona kipaji chake na kuamua kumsupport. Angalia picha.