Joe Budden anaendelea kumuandama rapa Drake baada ya kuponda album yake mpya ya ‘Views From The Six’ sasa anamtuhumu Drake kumdiss P Did...
Joe Budden anaendelea kumuandama rapa Drake baada ya kuponda album yake mpya ya ‘Views From The Six’ sasa anamtuhumu Drake kumdiss P Diddi kwenye wimbo wake mpya wa 4 AM In Calabasas.
Drake na Diddy waliwahi kuwa na beef December 2014 kutokana na Drake kufanya wimbo kwenye beat ambayo ilitakiwa kuwa ya P Diddy na kuimba wimbo wa “0 To 100” , ila baadae walipatana mwaka 2015.
Kwenye wimbo mpya wa “4PM,” Drake ametumia flow ya wimbo wa Bad Boy huku akidai kuwa hata wasanii wakongwe walijaribu kumtignisha “The higher I get the less they accept me / Even had the OGs tryna press me, Ha-ha-ha-ha,” akicheka kama Diddy alivyocheka kwenye wimbo wake wa mwaka 1997 “Can’t Nobody Hold Me Down“.
Budden anasema hii ni diss kwa Puff, kupitia twitter “Can’t let a nigga grab the classic bad boy loop, then sing all your hits as he disses u & not fire back lol for HipHop!”