Mkali wa hip hop kutoka Arusha,Joh Makini amefichua siri kuwa msanii wa Nigeria ,Davido ameimba kwa kiswahili kiitikio chote cha ngoma y...
Mkali wa hip hop kutoka Arusha,Joh Makini amefichua siri kuwa msanii wa Nigeria ,Davido ameimba kwa kiswahili kiitikio chote cha ngoma yao walioifanya pamoja ambayo bado haijatoka.
Joh Makini alifichua siri hiyo kwenye kipindi cha The Base cha ITV alipoulizwa kwanini anapenda kupenyeza Kiswahili kwenye verse za wasanii wa nje anaofanya nao kolabo ambapo yeye alidaai anafanya hivyo kama njia mojawapo ya kutangaza lugha ya Kiswahili.
“Mimi huwa n tumia hizo platfom (za kimataifa) kuitangaza lugha yetu ili iende mbali ,kwa sababu ni moja ya lugha kubwa za dunia na ni moja ya lugha zinazo flow vizuri sana kwenye muziki ..watu wengi tunaofanya nao kolabo wanataka kuijua wanaomba tuwaandikie,kwa mfano Davido tulimwandikia Chorus tukamtumia na akaimba vile vile kwa kiswahili kote hakubadilisha hata neno” alifunguka Joh Makini.