http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Roma Mkatoliki afungiwa kufanya muziki


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki amefungiwa kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa ms...

JAY-Z athibitisha mamake ni mpenzi wa jinsia moja
TID, Quick Rocka na OMG wamalizana
Umesikia alichokisema Wema Sepetu kuhusu shepu yake?
Msanii wa muziki wa Hip Hop bongo Roma Mkatoliki amefungiwa kufanya shughuli za muziki kwa muda wa miezi sita kwa kile kilichodaiwa msanii huyo kudharua wito wa BASATA na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Akiongea na waandishi wa habari Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Juliana Shonza amesema kuwa amechukua maamuzi hayo kutokana na kumwita msanii huyo ili aweze kufika kwenye mkutano huo lakini hakuweza kufika wala hakutoa taarifa yoyote ile.
"Roma Mkatoliki alipigiwa simu na BASATA hapokei na anatumiwa message anasoma lakini hajibu kitu, kwa hiyo kimsingi hilo ni kosa kwa sababu tumemuita si kama tumekurupuka bali Roma Mkatoliki aliutoa wimbo wake muda kidogo unaitwa Kibamia kimsingi ule wimbo ameimba matusi matupu na ni wimbo ambao kiasi fulani unadhalilisha kwa sababu mtu unapozungumzia kibamia huitaji kujiuliza kibamia ni nini kila mtu anajua maana ya kibamia, mimi siamini hata mtu ambaye yupo hivyo anakuwa amependa" 
Juliana aliendelea kutoa ufafanuzi kuhusu suala la Roma Mkatoliki
"Nakumbuka mwaka jana nilikuagiza Mkurugenzi wa BASATA kwamba umwite Roma Mkatoliki ukae naye chini, kwenye onyo lake la kwanza mwambie afanyie marekebisho huo wimbo na uzuri BASATA walimwita wakaa naye chini wakamwambia kasoro za wimbo wake na kutakiwa kufanya marekebisho ya wimbo huo ikiwepo jina lenyewe la Kibamia, pamoja na baadhi ya matusi ambayo yapo kwenye huo wimbo. Roma Mkatoliki alikubali na kusema ataenda kufanyia marekebisho hizo sehemu cha kusikitisha mpaka saizi napoongea hakuna ambacho kimefanyika na mbaya zaidi wimbo huo unaendelea kupigwa kwenye vyombo vya habari"
"Roma Mkatoliki amedharau maagizo ambayo alipewa na BASATA na kwa sababu tumemwita leo na hajafika bila taarifa yoyote hivyo amedharau wito, mimi kama Naibu Waziri wa Habari pamoja na BASATA tumekubaliana kwamba huyu ndugu Roma Mkatoliki tunampa adhabu kwa mujibu wa Katiba na kanuni, hivyo tunamfungia kwa muda wa miezi sita ndani ya muda huo wa miezi sita hakuna kufanya kazi yoyote ya sanaa, hakuna kutoa wimbo wowote, hakuna kufanya show sehemu yoyote, huo wimbo moja kwa moja tunaufungia" alisisitiza Shonza

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Roma Mkatoliki afungiwa kufanya muziki
Roma Mkatoliki afungiwa kufanya muziki
https://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/03/01/Roma%20Mkatoliki.jpg?itok=3sVI6ZU7×tamp=1519913095
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/roma-mkatoliki-afungiwa-kufanya-muziki.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/roma-mkatoliki-afungiwa-kufanya-muziki.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy