Msanii muziki wa staili ya Takeu amabe anafanya vizuri kwa sasa na kibao chake kipya cha 'Tuheshimiane', Mr Nice amefunguka na ...
Msanii muziki wa staili ya Takeu amabe anafanya vizuri kwa sasa na
kibao chake kipya cha 'Tuheshimiane', Mr Nice amefunguka na kumchana
Dudu Baya kuwa ameyumba kiuchumi ndio maana anasingizia kuacha pombe
bila ya kusema ukweli unaomkabili.
"Mimi nina mpongeza kutokana sina sababu ya kumsikitia kwasababu ni maamuzi yake yeye mwenyewe, labda ameona mwili wake hauwezi kuhumudu, uchumi vitu kama hivyo. Kwa hiyo usikae kumpongeza tu muda mwingine anapaswa apewe pole maana anaweza akawa yupo katika matatizo makubwa mpaka yakamfanya akashindwa kununua hiyo pombe",amesema Mr. Nice.
Pamoja na hayo, Mr. Nice ameendelea kwa kusema "huwenda Dudu Baya ameteteleka kiuchumi ndio maana anasingizia kuacha pombe lakini mimi naendelea na maisha yangu, kuburudika ni moja ya sehemu ya maisha yangu maana wote hatuwezi tukafanana".