‘...
‘A Boy From Tandale’ ndio jina litakalokuwa likiibebe album
ya mtumbuizaji huyo wa kimataifa kutoka Tanzania Naseeb Abdul Juma
maarufu kwa jina la Diamond Platnumz.
Muda mrefu sasa tangu Platnumz alipoanza kuizungumzia Album yake mpya na sasa kuna kila dalili ya kuashiria kuwa imekwisha kamilika na kinachosubiriwa ni muda tu wa kutoka ambao haujawekwa wazi na uongozi unaomsimamia Diamond Platnumz.
Hata hivyo, hivi karibuni Diamond ameonekanam akiwa anafanya Video na msanii mkubwa duniani Rick Ross huko mjini Miami nchini Marekani ambako Diamond aliongozana na msanii kutoka WCB Ray Vanny katika tuzo za Afrimma zilizotolewa Dallas, Texas Marekani
Kwa muonekano wa ‘Cover’ ya Album hiyo inaashiria kuwa ni Album ambayo itakuwa na hamasa kubwa kutokana na uhalisia wa maisha ya Diamond alikotoka mpaka sasa alipo.
Album hii ya A boy From Tandale itakuwa ni Album ya pili kutoka kwa Diamond na itasaidia kurusdisha mfumo wa Album kwa wasanii wengi wa hapa nyumbani ambao wamekuwa wanahofia sana soko la Album.
Diamond akitoa Album yake mwaka huu atakuwa ameungana na Chegge, Ben Pol, Navy Kenzo na Lady Jay Dee ambao wote wamekwisha toa Album zao mwaka huu.