http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mtumbwi Wazama na Kuua Watatu


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Watu watatu wakiwamo watoto wadogo wawili wamekufa huku wawili wakinusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye mto Ruvu...

Chadema yawekewa ulinzi kila kona Dodoma ....Polisi watoa maagizo maalumu kwa wamiliki wa nyumba za wageni, Viongozi wa Bavicha wapandishwa kizimbani
Mwalimu acharangwa mapanga kwa kumpa mimba mwanafunzi
Wanafunzi Chuo Kikuu Kizimbani Kwa Mauaji

Watu watatu wakiwamo watoto wadogo wawili wamekufa huku wawili wakinusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kuzama kwenye mto Ruvu, walipokuwa wakijaribu kuvuka kutoka Vigwaza kwenda Mlandizi mkoani Pwani.


Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Jonathan Shana alisema licha ya watu hao kubainika kufa, nahodha wa mtumbwi huo hajulikani alipo. Shana alisema ajali hiyo imetokea Jumamosi saa 4:00 asubuhi kwenye mto Ruvu wilaya ya kipolisi Chalinze.


“Ajali hiyo imepoteza maisha ya watoto wawili ambao ni Nusrat Haji miezi minne na Feisal Hamza mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu pamoja na Sikuzani Musa (41), ambaye mwili wake bado haujapatikana,” alisema Kamanda Shana.


Kamanda Shana aliwataja walionusurika ni Zuwena Ramadhan (29) na Tero Mziray (20) ambapo dereva wa mtumbwi huo hajulikani alipo na inaaminika hakufa maji.


“Chanzo cha mtumbwi huo kuzama bado kinachunguzwa na miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi,” aliongeza.


Aliwataka wamiliki wa vyombo hivyo kuhakikisha vinakuwa kwenye hali nzuri ili kuepukana na ajali kama hizo ambazo zinapoteza uhai wa watu kutokana na ubovu.A

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mtumbwi Wazama na Kuua Watatu
Mtumbwi Wazama na Kuua Watatu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMzRJQ9Lqr7Pw3vc3tq5yQFc2CfFy5eHhXiPUL98obqD5NlbxS82ps9qtYgtkzPyi5eLIa9QByfNK9Y0fD6T9YCMNt9XBCJJwPUOR_qbFZ-ZhUapnWQrR4Upv8qcol5t0d4x9QlHs1K_li/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMzRJQ9Lqr7Pw3vc3tq5yQFc2CfFy5eHhXiPUL98obqD5NlbxS82ps9qtYgtkzPyi5eLIa9QByfNK9Y0fD6T9YCMNt9XBCJJwPUOR_qbFZ-ZhUapnWQrR4Upv8qcol5t0d4x9QlHs1K_li/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/mtumbwi-wazama-na-kuua-watatu.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/mtumbwi-wazama-na-kuua-watatu.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy