http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Vifaru vya Urusi vinavyotia wasiwasi mataifa ya Nato barani Ulaya


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Urusi imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya mfumo wake wa kukabiliana na vifaru wakati wa vita. Vifaru hi...

SNURA AKANUSHA KUFUNGIWA YEYE NA WIMBO WAKE
VIDEO YA SNURA AKIWAOMBA WATANZANIA RADHI KWA KUWADHALILISHA WANAWAKE KUPITIA NYIMBO YAKE.. 'CHURA'
RAISI MAGUFULI, AMTEUA DKT. ASHA ROSE MIGIRO KUWA BALOZI WA TANZANIANCHINI UINGEREZA

Urusi imeunda vifaru vipya ambavyo vimeifanya Norway kuanza kufikiria upya mfumo wake wa kukabiliana na vifaru wakati wa vita.

Vifaru hiyo vipya vya Urusi kwa jina Armata T-14 vinaundwa vikiwa na teknolojia ya Kinga Dhidi ya Makombora (APS).

Lengo la teknolojia hiyo ni kuwezesha vifaru hivyo kutoharibiwa na makombora mengi yaliyoundwa kukabiliana na vifaru, yakiwemo yale aina ya Javelin yanayoundwa Marekani, ambayo yanatumiwa na jeshi la Norway.

Brigidia Ben Barry wa taasisi kuhusu usalama wa kimataifa ya International Institute for Strategic Studies (IISS) mjini London anasema mataifa yanfaa kuanza kufikiria upya teknolojia yake ya kukabiliana na makombora.

Anasema mataifa mengi ya Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi (Nato) hayajagundua tatizo linalowakabili.

Teknolojia ya APS inatishia kufanya silaha nyingi za kukabiliana na vifaru kutofanikiwa, na mataifa mengi ya Magharibi hayajaanza kujadiliana kuhusu hatua za kuchukua.

Anasema baadhi ya nchi zinafanya utafiti na majaribio kivyake kuweka mfumo huo wa APSkwenye vifaru vya mataifa hayo.

"Lakini yanakosa kuzingatia matokeo ya teknolojia hii kwa mfumo wao wa kukabiliana na vifaru,2 anasema.

Norway ni moja ya nchi za kwanza kukumbana na hatari hii.
Nchi hiyo inapanga kutumia krona 200-350m (£18.5-32.5m; $24-42m) kubadilisha makombora yake ya Javelin na "kudumisha uwezo wake wa kukabiliana na vifaru".

"Kuna haja ya kuwa na makombora ambayo yanaweza kupenga mfumo wa APS."




Adui anarusha kombora au mzinga kushambulia kifaru
Mfumo kwenye kifaru unagundua kuna tishio njiani
Teknolojia ya rada inahesabu njia na pahali palipolengwa
APS inarusha kombora la kuharibu kombora au mzinga
Kombora au mzinga wa adui unaharibiwa
Teknolojia ya APS imebadilisha mambo katika historia ya kuangazia kushambulia na kujilinda wakati wa vita.

Katika vipindi fulani, kuna moja ambayo ilikuwa mbele.
Zamani, vifaru visivyoweza kupenya risasi vilitawala, lakini makombora nayo yakaimarisha na kumaliza ubabe huo.

Tangu Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, vifaru vimeendelea kutawala katika uwanja wa vita.
Vifaru hata hivyo, huwa vinaweza kuharibiwa na makombora au mabomu ya vifaru vingine vikiwa karibu.

Lakini kulikuwa pia na tishio kutoka kwa silaha nyingine, mfano makombora ya kurushwa kutoka mbali au kutoka kwa ndefe, jambo ambalo ndilo teknolojia ya APS imeundwa kukabili.







Israel ni miongoni mwa mataifa ambayo yamekuwa yakiongoza katika teknolojia ya kujikinga na vifaru vyake aina ya Merkava hutumia teknolojia hii.

Vifaru hivyo vilitumiwa kukabiliana na wapiganaji wa Kipalestina ukanda wa Gaza.

Mfumo huo wa Israel pia unachunguzwa na Wamarekani, Uingereza pia imeanza kutafakari uwezekano wa kustawisha teknolojia kama hiyo.

Uholanzi imeamua kutumia teknolojia nyingine, pia kutoka Israel, kukinga vifaru vyake.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Vifaru vya Urusi vinavyotia wasiwasi mataifa ya Nato barani Ulaya
Vifaru vya Urusi vinavyotia wasiwasi mataifa ya Nato barani Ulaya
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi90pjCvYdl_Hmhh7rik6hDvzkiz4M5sa7m-vhWCMPZSXIMlHCd9crsPc8FkBZNxMshLAlRbzFaKAf8voXR-dOdNehHbJsQzxO62BmdsSTe3-p0CIFU_cFzLJkQ_RUePrsYqRJ7aqt1340/s400/_96257868_armatatankt14afp9may17.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi90pjCvYdl_Hmhh7rik6hDvzkiz4M5sa7m-vhWCMPZSXIMlHCd9crsPc8FkBZNxMshLAlRbzFaKAf8voXR-dOdNehHbJsQzxO62BmdsSTe3-p0CIFU_cFzLJkQ_RUePrsYqRJ7aqt1340/s72-c/_96257868_armatatankt14afp9may17.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/05/vifaru-vya-urusi-vinavyotia-wasiwasi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/05/vifaru-vya-urusi-vinavyotia-wasiwasi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy