Baraza la vijana la Mkoa wa Arusha BAVICHA Jana limefanya ziara katika Jimbo la Arumeru Magharibi kwenye kata ya Oldonyosambu na kukutana ...
Baraza la vijana la Mkoa wa Arusha BAVICHA Jana limefanya ziara katika Jimbo la Arumeru Magharibi kwenye kata ya Oldonyosambu na kukutana na diwani na viongozi wa kata hiyo,ambapo walifanya kikao cha pamoja na kufungua tawi eneo hilo.
Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha Mhe. Exaud Mamuya pamoja na katibu wa BAVICHA Mkoa wa Arusha Mhe.Jenipher Mwasha viongozi wengine walioambatana nao ni Pamoja na katibu wa Jimbo la Arumeru Magharibi Mhe.Charles Adieli na katibu wa baraza la wazee pamoja na mwenyekiti wa BAVICHA Jimbo la Arumeru Magharibi.