http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Waziri Mkuu wa Ethiopia kutua nchini Leo


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajiwa kuwasili nchini kesho, Machi 31 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kufuatia mw...

Kigogo aweka majina hewa mradi wa Tasaf
Mwanasiasa wa miaka 90 kuoa mwanamume Marekani
Vyama vyakacha kuwasilisha hesabu

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn anatarajiwa kuwasili nchini kesho, Machi 31 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Afrika Masharika, Dkt. Suzan Kolimba alipokuwa Akizungumza na waandishi wa habari.


Alisema kuwa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn imetokana na mkutano kati yake na Rais Dkt. Magufuli uliofanyika baada ya mkutano wa kawaida wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika hivi karibuni huko nchini Ethiopia.


Alisema kuwa madhumuni ya ziara hiyo ni pamoja na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.


“Mahusiano ya Tanzania na Ethiopia ni mazuri, Ethiopia imeonesha nia ya kufungua Ubalozi wake hapa nchini hivi karibuni. Kwa sasa Ethiopia inawakilishwa nchini na Balozi wake aliyepo Nairobi nchini Kenya” alisema Naibu Waziri Kolimba.


Wakati wa ziara hiyo,Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn atakutana na Rais Dkt. John Magufuli kwa mazungumzo, watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari.


Aprili 01 mwaka huu, Waziri mkuu huyo wa Ethiopia atatembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa Bandarini hapo, Dessalegn na ujumbe wake wataondoka siku hiyo hiyo kurejea Ethiopia.


Hata hivyo, Mwaka 2015 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Dessalegn alitembelea Tanzania na kushiriki uzinduzi wa Kiwanda cha kutengeneza dawa za kuua viluwi luwi vya mbu wanaoeneza Malaria kilichojengwa Kibaha, Pwani kwa ufadhili wa Serikali ya Cuba.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Waziri Mkuu wa Ethiopia kutua nchini Leo
Waziri Mkuu wa Ethiopia kutua nchini Leo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQtnLvmwo7PqS6Vm0ZmyYNkFzc4QENf5rhohXnA3MChy4J6ErXUqM3ITaCfv5-3vRpBv60aj7NX99qWSwjqs9dgyN-O-9FXyXy3k-SAG72pU250PgvPsiIS_tKuCdPFPmiyi-gYXpadix3/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQtnLvmwo7PqS6Vm0ZmyYNkFzc4QENf5rhohXnA3MChy4J6ErXUqM3ITaCfv5-3vRpBv60aj7NX99qWSwjqs9dgyN-O-9FXyXy3k-SAG72pU250PgvPsiIS_tKuCdPFPmiyi-gYXpadix3/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/waziri-mkuu-wa-ethiopia-kutua-nchini-leo.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/waziri-mkuu-wa-ethiopia-kutua-nchini-leo.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy