http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Agosti 2 katika mikoa yote

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo ya bidhaa za mafuta aina ya petroli kwa Agosti , ambazo zimeend...


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetoa bei kikomo ya bidhaa za mafuta aina ya petroli kwa Agosti , ambazo zimeendelea kushuka kwa miezi minne mfululizo kuanzia Aprili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Godwin Samwel, bei zitakazoanza kutumika leo zimeshukwa kwa Sh36 na Sh44 kwa lita ya petrol na dizeli mtawalio.

Taarifa hiyo inasema kwamba tofauti ni katika mafuta ya taa ambapo bei yake imeongezeka kwa Sh24 kwa lita, hali iliyosababishwa na kuongezeka kwa gharama ya usafirishaji wa bidha katika mfumo wa Uagizwaji wa Mafuta kwa Pamoja (BPS).

Wastani wa matumizi ya mafuta kwa siku ni lita milioni tano, milioni tatu na 100,000 kwa dizeli, petrol na mafuta ya taa, sawia.

Kutokana na bei hizo mpya, kuanzia leo lita moja ya petrol katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,978 kutoka ilivyokua mwezi uliopita ya Sh2,014, wakati lita ya dizeli sasa itauzwa Sh1,830 kutoka Sh1,874 na mafuta ya taa yatapanda mpaka Sh1,830 kutoka Sh1,806 kwa lita kwa mwezi uliopita.

Mhandisi Samweli amesema kwa Mkoa wa Tanga, hakutakuwa na mabadiliko kwa petroli na dizeli kwa sababu hakuna mzigo uliopokelewa kupitia bandari ya Tanga kwa mwezi wa saba 2017. Hii itafanya bei za bidhaa hizo kwa mkoa huo kubaki kama zilivyokua kwa mwezi wa saba 2017.

“Pia, kwa kuwa hakuna bidhaa mpya ya mafuta ya taa iliyoingizwa kupitia bandari ya Tanga, wafanyabiashara wanashauriwa kuchukua bidhaa hiyo kutoka mkoa wa Dar es Salaam na pia, bei ya mafuta ya taa kwa mkoa wa Tanga zitategemea na gharama za mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji kutoka Dar es Salaam hadi Tanga”, amesema.

Kwa upande wa waendesha magari ambao wangependa kupata bei za mafuta, wanaweza kupata bei kikomo kwa kutumia simu ya mkononi kwa kupiga *152*00 na kisha kufuata maelekezo.


Taarifa ya Ewura inasema puia kuwa kampuni za kuuza mafuta ziko huru kuuza bidhaa zao katika bei ya ushindani yenye faida, isipokuwa wazingatie kuwa bei hizo hazizidi bei elekezi.
==> Hapo chini ni Taarifa nzima ya EWURA

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Agosti 2 katika mikoa yote
Bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Agosti 2 katika mikoa yote
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdgc2VaxnsRVrEl_3L5-uYxAYhfoNOvNL1WgCv3iIfy5ucV8m_VHybiMrtAN1It9BDAz1_uMts0O6Wxj_UCwPAOno3_PVq-k919yWXByKOoG_SkPc4buZLUI_4xVqSISGGvZq_pi57yDrA/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdgc2VaxnsRVrEl_3L5-uYxAYhfoNOvNL1WgCv3iIfy5ucV8m_VHybiMrtAN1It9BDAz1_uMts0O6Wxj_UCwPAOno3_PVq-k919yWXByKOoG_SkPc4buZLUI_4xVqSISGGvZq_pi57yDrA/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/bei-mpya-za-mafuta-zilizoanza-kutumika.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/bei-mpya-za-mafuta-zilizoanza-kutumika.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy