http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mfanyabiashara Yusuf Manji apiga hodi Mahakama Kuu


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ...

Serikali kuwapunguzia muda wa masomo madaktari
Mwandishi nguli wa habari za uchunguzi auawa
VIDEO.ASKOFU: WANAOSEMA MAGUFULI AONGEZEWE MUDA NI WAPUUZI


Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.
Manji yuko kwenye matibabu Hospitali ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana. Februari 20 mwaka huu, alipelekwa ofisi ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa madai ya kuingia nchini kinyume cha sheria.


Katika kesi hiyo wajibu maombi hayo ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo aliyefungua kesi ya maombi hayo, anataka Mahakama iagize maofisa uhamiaji na polisi kumfikisha mahakamani ili iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.

Katika hati ya maombi hayo, Ndusyepo anadai kuwa alimtembelea mteja wake hospitali ya Aga Khan Februari 17 mwaka huu na kukuta maofisa wa Uhamiaji wakimsubiri mteja wake wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa kwa mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa siyo raia wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai kuwa alitoa maelezo kwa maofisa Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.


Kwa ufupi
Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mfanyabiashara Yusuf Manji apiga hodi Mahakama Kuu
Mfanyabiashara Yusuf Manji apiga hodi Mahakama Kuu
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3851596/highRes/1591000/-/maxw/600/-/61wd57/-/pic+manji.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/mfanyabiashara-yusuf-manji-apiga-hodi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/03/mfanyabiashara-yusuf-manji-apiga-hodi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy