Richard Bezuidenhout ambaye ni mshindi wa big brother II mwaka 2007 na mwigizaji wa filamu amedai kuwa wasanii wengi wa filamu wA bongo ...
Richard Bezuidenhout ambaye ni mshindi wa big brother II mwaka 2007 na mwigizaji wa filamu amedai kuwa wasanii wengi wa filamu wA bongo wanakurupuka kufanya kazi ndio maana tasnia ya muvi Tanzania Haifiki mbali.
Akiongea na Global Tv online Richard amewataka wasanii wa bongo kuiga mfano kwa nchi zilizoendelea ambapo kazi hiyo ni taaluma ambayo watu huenda shule kusomea.
“watengezaji wa bongo muvi sasa hivi wanakurupukia fani,watu hawaiiehismu bongo muvi kama kazi.Ukiangalia nchi zilizoendea watu wanachukulia filamu kama kazi, wanaenda kusomea kabisa..hapa kwetu watu wanachaguana tu hata kama mtu hajasoma mwisho wa siku unakuta soko limejaa fujo.” alisema Richard ambaye yuko mbioni kuachia muvi yake mpya.