http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mshitakiwa Mauaji ya Mwangosi Ana Kesi ya Kujibu


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

M ahakama  Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali ombi la kumuachia huru mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo ch...

Boti yazama na wahamiaji Ugiriki
Vyama vya Upinzani Kufanya Maandamano Nchi Nzima Kupinga Kusimamishwa Wabunge wake 7
Mwakyembe Ataka Mishahara na Posho za Wabunge wa UKAWA Zifutwe.........Keissy Awafananisha na Watumishi HEWA


Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imetupilia mbali ombi la kumuachia huru mtuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Channel 10 mkoani humo, Daudi mwangosi na badala yake imesema ana kesi ya kujibu.

Akitoa uamuzi wa ombi hilo mahakamani hapo jana, Jaji Paulo Kihwelo, alisema mahakama imeona mtuhumiwa huyo ana kesi ya kujibu na anatakiwa  kupeleka mashahidi makamanani.
  
Akizungumzia uamuzi huo, wakili wa upande wa utetezi, Rwezaura Kaijage, alisema wameridhika na watatoa ushahidi wakiwa na shahidi mmoja ambaye ni mtuhumiwa mwenyewe.
  
“Utetezi tumeridhika na uamuzi wa mahakama, shahidi atakuwa mmoja na ni mtuhumiwa mwenyewe, lakini tunaiomba mahakama yako tukufu ushahidi huo utolewe kwa njia ya kiapo,” alisema.
  
Kaijage aliomba utetezi huo utolewe leo kuanzia saa 3: 00 asubuhi. Kwa upande wa wakili wa Jamhuri, Ladislaus Komanya na mwenzake Sunday Hyera, walisema hawana pingamizi lolote la ombi hilo kuwa utetezi utolewe leo.
  
Ulinzi Mkali Mahakamani
Kabla ya Jaji kuingia kwenye chumba cha mahakama, ulinzi mkali wa polisi ulitawala nje na ndani ya mahakama, wakiwamo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kuzingira eneo hilo.
  
Aidha, waandishi wa habari walipata wakati mgumu kutekeleza kazi yao baada kunyimwa kuingia ndani ya chumba cha mahakama kwa kisingizio kuwa kesi haijaanza, hali iliyolazimu Msajili wa Mahakama hiyo, Ruth Massam, kuingilia kati na kuwataka polisi kuacha lakini hawakumsikiliza.
  
Baada ya mvutano huo, waandishi walikaguliwa na kisha kuruhusiwa kuingia, lakini hali iliendelea kuwa ngumu ndani ya chumba cha mahakama kiasi cha kutishiwa kuvunjiwa vitendea kazi vyao na baadhi ya polisi.
  
Hata hivyo, waaandishi waliendelea kutekeleza majukumu yao hadi kesi ilipoanza.
  
Baada ya Jaji Kihwelo kuahirisha kesi hiyo, mtuhumiwa alishuka kizimbani kimgongo mgongo ili asionekane sura, huku askari wenzake wakimfunika kwa kitambaa na kitenge kichwani, pamoja na bahasha ya kaki. Askari zaidi ya 30 walimzingira ili asipigwe picha.
  
Mwangosi aliuawa Septemba 2, 2012 kwenye ufunguzi wa matawi ya Chadema katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mshitakiwa Mauaji ya Mwangosi Ana Kesi ya Kujibu
Mshitakiwa Mauaji ya Mwangosi Ana Kesi ya Kujibu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgM_zYfrHGVpav9FBam9KghSpFe-sL7PXVm_Rjt2wS4rgu6uToJr0Rp-P2pasE5r61PufKDwz_pfC28KzwNqKqk6wUAQTTiiFkyUpyEOqepMeEyI2HJOCOROckjP72rhzC9ehEE4AxwMXjy/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgM_zYfrHGVpav9FBam9KghSpFe-sL7PXVm_Rjt2wS4rgu6uToJr0Rp-P2pasE5r61PufKDwz_pfC28KzwNqKqk6wUAQTTiiFkyUpyEOqepMeEyI2HJOCOROckjP72rhzC9ehEE4AxwMXjy/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/mshitakiwa-mauaji-ya-mwangosi-ana-kesi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/06/mshitakiwa-mauaji-ya-mwangosi-ana-kesi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy