JESHI la Polisi Mkoani Arusha limekamata vitu mbalimbali vya thamani ikiwemo bunduki ya kivita aina ya AK 47,magari mawili ya wizi,pikipiki...

JESHI la Polisi Mkoani Arusha limekamata vitu mbalimbali vya thamani ikiwemo bunduki ya kivita aina ya AK
47,magari mawili ya wizi,pikipiki saba na vifaa mbalimbali vya
kielektroniki vilivyokuwa vimeporwa katika maeneo mbalimbali mkoani hapa
Aidha katika matukio.hayo jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni wahalifu 10 wanaohusishwa na uporaji huo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Ramadhani Ng'anzi amewaambia
waandishi wa habari ofisini kwake mapema leo Mey 29 kuwa kukamatwa kwa vitu hivyo
kunafuatia operesheni kali ya jeshi hilo kukabiliana na uhalifu
iliyoanza mei 25 mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha
Amesema kuwa katika tukio la kwanza mnamo tarehe 26 mei mwaka huu
katika katika kijiji cha Naan Wilayani Ngorongoro Polisi walikamata
bunduki hiyo aina ya AK 47 ikiwa na risasi 4 kwenye magazine ikiwa
imefichwa kichakani.
“Bunduki hii ilikuwa inatumika katika matukio mbalimbali ya unyanganyi
wa kutumia silaha na uwindaji haramu ambapo polisi tunaendelea
tunaendelea na juhudi za kumtafuta mtuhumiwa huyo pamoja na mtandao wa
wahalifu wanaotumia silaha hiyo”alisema Kamanda huyo wa Polisi.
Aliongeza kuwa katika operesheni hiyo polisi walifanikiwa kukamata
magari mawili ya wizi ambayo ni Prado aina ya TX Land Cruiser yenye
namba za usajili T279 CRQ na Toyota Grand Mark II namba T702 BHN yote
yakiwa meupe.

Kamanda Ng’anzi aliendelea kueleza kuwa katika maeneo ya Wilaya za
Arusha mjini,Monduli na Arumeru polisi imekamata pikipiki 7 za aina
mbalimbali ambapo vitu vyote hivyo vinashiliwa katika kituo kikuu cha
polisi Arusha.
“Mali nyingine za wizi zilizokamatwa na vifaa vya kielektoniki
zikiwemo TV Flat Screen za aina mbalimbali ,Kamera,Redio,
Ipad,Deki,Vingamuzi,PasiMicrowave,Laptop za aina mbalimbali,mablanketi
na mapazia pamoja na mabegi ya nguo zikiwemo fedha taslimu shilingi
915,000”aliongeza kamanda huyo wa polisi
Aliongeza kuwa katika matukio hayo polisi inawashikilia watu 1o kwa
matukio hayo huku ikiendelea kuwatafuta wengine ambapo ametoa rai kwa
wakazi wa arusha walioibiwa vitu vyao kujitokeza katika makao makuu ya
polisi kwa ajili ya kuvitambua.
…



