http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

WABUNGE WAMPA MAKAVU WAZIRI KITWANGA ALIYETUMBULIWA JIPU KWA ULEVI


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kutimuliwa nafasi hiyo kwa ulevi, wabunge na...

Wapinzani Waungana Kumng'oa Mugabe Uchaguzi Mkuu Ujao
Taarifa ya ajali ya treni na daladala ya kutoka Gongo la Mboto Alfajri leo Aprili 19, 2017.
SIKILIZA KIPINDI CHA RADIO , HOT BOX PIA WAWEZA KUDOWNLOAD

Siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kutimuliwa nafasi hiyo kwa ulevi, wabunge na wasomi wameendelea kumbana zaidi wakisema hatua hiyo ya Rais imechelewa.

Wapinzani wamekuwa wakimtaka Rais amuondoe kwenye nafasi hiyo kutokana na kuhusishwa na Kampuni ya Infosys ambayo ilitoa ushauri kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises iliyopewa zabuni ya kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole (AFIS) katika vituo vya polisi.

Wakati wasomi wakisema hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi huo ulikuwa sahihi na swali ambalo Kitwanga hakulijibu vizuri kutokana na hali ya ulevi, litapaswa kujibiwa upya baada ya wabunge kuomba mwongozo wa swali hilo.

Majaliwa alisema Rais ametengua uteuzi wa Kitwanga kuanzia juzi baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi.

“Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake...,”alisema Majaliwa.

Alisema uamuzi wa Rais Magufuli umefuata kanuni za utumishi wa umma ambazo zinakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

Ingawa Majaliwa hakutaja kanuni hiyo, Kifungu cha 34 cha Sheria ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2002 pamoja na Kanuni ya 65 (1) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003, kinasema, “Watumishi wa Umma wanapaswa kuepuka tabia ambayo inavunja heshima ya utumishi wao kwa umma hata wanapokuwa nje ya mahali pa kazi."

Tabia inayoweza kuvunja heshima hiyo inatajwa kuwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, ulevi, kukopa kwa kiwango ambacho hawawezi kurejesha na mwenendo mbaya na kujihusisha na vitendo vyovyote viovu mbele ya jamii.

Bunge kuchukua hatua?
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah alipoulizwa adhabu ambazo mbunge anaweza kupata iwapo ataingia bungeni akiwa amelewa, alisema wanaoweza kujibu hilo ni Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni na Mnadhimu wa Serikali Bungeni, Jenister Mhagama.

Hata hivyo, Mhagama ambaye ni Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, alisema hawezi kueleza hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa kuwa tayari Rais ameshachukua uamuzi wa kutengua uteuzi huo.

“Ila Bunge lina taratibu na kanuni zake, nadhani Spika au katibu wa Bunge watakueleza vizuri,” alisema Mhagama.

Spika Job Ndugai hakupatikana kwenye simu, huku Naibu Spika simu yake iliita bila kupokewa.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel alisema: “Kanuni hazijaweka utaratibu wa mbunge anayeingia bungeni amelewa ila kuhusu suala la Kitwanga ni la nidhamu ya utumishi wa umma, labda kama atafanya jambo ambalo siyo la kawaida.” 

Wabunge  'Wampa Makavu'
Wabunge wa CCM na upinzani nao walitoa maoni kuhusu hatua hiyo wakisema ilikuwa haki kwa waziri kuachishwa kazi kwani alikuwa ametia aibu Serikali huku wakimpongeza Rais Magufuli kuwa yuko makini. 

Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya alisema alichokifanya Magufuli ni kizuri na kwa sababu waziri huyo alishindwa kujiwajibisha mwenyewe.

Sakaya ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), alisema kitendo cha Dk Magufuli kumtimua mtu wake wa karibu, ni ishara tosha kuwa amedhamiria kuwasaidia wanyonge na kuwatahadharisha mawaziri wengine kuwa makini na kazi zao.

“Huyu waziri angeweza kujiwajibisha mwenyewe kutokana na makandokando yake, lakini akachelewa na sasa amekutana na mkono wa Rais kwa kuwa hataki uchafu, ni kweli jana (juzi) Kitwanga alikuwa amelewa wala siyo utani,” alisema Sakaya.

Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa (CCM), alimpongeza Rais Magufuli kwa kuona jambo hilo akisema, haiwezekani kufanya kazi na watovu wa nidhamu hasa katika masuala ya ulevi.

Ndasa alisema kulewa ni sehemu ya utovu wa nidhamu lakini inakuwa shida zaidi pale viongozi wenye dhamana wanapolewa tena nyakati za kazi kwani inakuwa ni mfano mbaya, hivyo waziri huyo amevuna alichopanda.

Ali Saleh (Malindi – CUF) alisema Kitwanga alichelewa kuondolewa katika nafasi yake kwani alikuwa ni miongoni mwa majipu. 

Alisema waziri huyo alipaswa kuchunguzwa na Ikulu mapema baada ya kuanza kwa kelele za wapinzani, lakini watu wengi walishindwa kumpa Rais habari za ukweli kuhusu waziri wake. 

Alisema kutumbuliwa kwa Kitwanga kusitafsiriwe kwa mambo ya ulevi pekee, maana wakuu wa mikoa na wilaya wataanza kufanya hivyo kwa uonevu kwa watu ambao watakuwa wamewanyima hata pombe vilabuni.

Joel Mwaka (Chilonwa – CCM) alimpongeza Rais Magufuli kuwa ni mtu anayeyaishi yale anayoahidi na hivyo kuwapa nafasi kubwa Watanzania na hasa wa chini huku akitahadharisha viongozi kuacha kuwadharau watu wa hali ya chini.

Suzan Kiwanga (Mlimba – Chadema) aliyeanzisha sakata hilo, aliwalaumu wasaidizi wa Kitwanga pamoja na dereva wake kwamba walishindwa kumshauri asiingie bungeni.

“Hakuwa katika hali ya kawaida, alilewa sana jamani hadi akashindwa kujibu swali, ningeshauri Rais aangalie sana kwa mawaziri wake kwani wengi wanaonekana kulewa hata madaraka na kujibu maswali kwa nyodo,” alisema Kiwanga.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alisema: “Eti wanadai ametumbuliwa sababu ya ulevi, hebu jiulize Waziri wa Mambo ya Ndani ana wasaidizi, ana mlinzi ana katibu ana dereva, huyu mtu aliyelewa kiasi hicho katibu alishindwa kumwambia maana kazi yao ni kumsaidia waziri asifanye mambo ya aibu. Sasa utawala uliofitinika hauwezi kusimama kamwe kuongoza taifa,” alisema Lema.

Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha alimpa pole Kitwaga akisema, hata yeye alikuwa anakunywa ndovu akiwa waziri lakini hakuwahi kutimuliwa.

“Namuonea huruma Kitwanga kwa sababu alikuwa haijui CCM, kama ni pombe mbona hata mimi nilikuwa nakunywa ndovu, nakijua chama hicho nilianzia chipukizi, hata umoja wa vijana, lakini niliamua kutoka,” alisema Masha.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : WABUNGE WAMPA MAKAVU WAZIRI KITWANGA ALIYETUMBULIWA JIPU KWA ULEVI
WABUNGE WAMPA MAKAVU WAZIRI KITWANGA ALIYETUMBULIWA JIPU KWA ULEVI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvBToB6vIM1HuhxdY6UFj86kXKqw6zFvRnSegjovX7DssIByz1NB5F1Ot3-jDSMnejbXcxQXXMjhyVzcgV89hlc1lGg8tuPYACIyvbJJ_SilJkYNpfk2XpwwX6OLQ4uNBv8uyGeyvBhiSS/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjvBToB6vIM1HuhxdY6UFj86kXKqw6zFvRnSegjovX7DssIByz1NB5F1Ot3-jDSMnejbXcxQXXMjhyVzcgV89hlc1lGg8tuPYACIyvbJJ_SilJkYNpfk2XpwwX6OLQ4uNBv8uyGeyvBhiSS/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/wabunge-wampa-makavu-waziri-kitwanga.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/wabunge-wampa-makavu-waziri-kitwanga.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy