Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina La Grace Anaely Mmari anayekadiliwa kuwa na umri wamiaka 40 amekutwa amekufa ndani ya chumbachake akiwa ame...
Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina La Grace Anaely Mmari anayekadiliwa kuwa na umri wamiaka 40 amekutwa amekufa ndani ya chumbachake akiwa amekaa kwenye kochi
Marehemu ambaye alikuwa akiishi peke yakekatika chumba alichokuwa amepanga katika Mtaa wa Tindigani ,kata ya Ungalimited jijini Arusha, mwili wake umekutwa ukiwa umeharibika kiasi cha kutoa harufu Kali
Mmoja ya jirani na marehemu huyo aitwaye ,Jakob Asenga amesema kabla ya mwili huokugundulika alisikia harufu Kali mithiri ya panya aliyefia ndani na alipoanza kufuatiliaaligundua harufu hiyo pamoja na Nzi ikitokeandani ya chumba hicho.
"Nilitoa taarifa kwa watu mbalimbali akiwemobalozi ambapo walifika na kuamua kuvunjamlango na kukuta mwili wa marehemu aliyekuwa amevalia suruwale ya Jinsi na blausinyeupe akiwa amekaa kwenye kochi huku pembeni yake kukiwa na jiko la mafuta na sufurialenye Nyama alilokuwa akipika "AnasemaAsenga
Aliongeza kuwa marehemu Mara nyingiamekuwa akiingia ndani ya chumba chake nakujifungia ndani na alikuwa hana ushirikianona mtu yoyote na Mara nyingi alikuwahazungumzi na jirani yoyote hata pale anaposemeshwa hujibu kwa ishara ya kichwa.
Mwenyekiti wa mtaa wa Tindiga Maria Kibonge ameeleza kuwa marehemu alipatataarifa juu ya tukio hilo leo Mei 27,majira ya saa 11.30 jioni na kwenda kushuhudia,ambapo alimkuta marehemu akiwa amekufa hukuakiwa amekaa kwenye kochi ambapo alitoataarifa kituo cha Polisi ambapo polisi walifikana kuuchukua mwili wake marehemu.
Naye kijana aitwaye John Mmari aliyejitambulisha kama Mdogo wa marehemu amethibitisha kuwa marehemu ni ndugu yake na kabla ya tukio hilo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwawa kifua.
Hata hivyo bado haijafahamika chanzo cha mauti hayo na lini mauti yalimfika marehemuHuyo ,mwili wake umehifadhiwa katikachumba cha maiti katika hospital ya Mkoa Mount Meru.
By Ngilisho