http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

MWALIMU WA MADRASA ADAIWA KUHUSIKA NA MAFUNZO YA KIGAIDI

Mwamvua Mwinyi,Pwani JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewakamata watoto 22 wa madrasa ya Arahma pamoja na mwalimu wa madrasa hiyo Ashura Said...


mush
Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewakamata watoto 22 wa madrasa ya Arahma pamoja na mwalimu wa madrasa hiyo Ashura Said(47) ambae alikuwa akiendesha mafunzo ya kigaidi kwa watoto hao,huko Kimarang’ombe ,kata ya Nianjema ,Bagamoyo.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kukuta bomu moja la moshi lenye namba G2020c.SS-STCS katika makazi anayoishi mwalimu huyo .

Akizungumzia tukio hilo,jana,kamanda wa polisi mkoani Pwani,Boniventure Mushongi,alisema Ashura anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusiana na kuhusika kuendesha mafunzo ya kigaidi kinyume na sheria.
Alieleza kuwa taarifa hiyo ilitolewa na raia wema juu ya mwenendo wa mwalimu huyo wa madrasa na baada ya kumfanyia upekuzi polisi walifanikiwa kukuta na bomu moja la moshi.
Kamanda Mushongi,alisema uchunguzi wa awali ulibaini makazi hayo yanamilikiwa na taasisi ya kiislamu iitwayo Akha Laagul Islam,iliyoyasiliwa kwa lengo la utoaji huduma kwa watoto yatima kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Dar es saalam ,Tanga,Handeni,Mlandizi na Bagamoyo kwa mkoa wa Pwani.
“Badala yake watoto hao wamekuwa wakitumika kwa mafunzo yasiyofaa kwa watoto wa kituo hicho”alisema kamanda Mushongi.
Hata hivyo alisema jeshi la polisi limewakata wattoto 22 ambao walikuwa wakijaribu kukimbia ambao kati yao 16 ni wakike na 6 ni wa kiume kwa ajili ya uchunguzi wa tukio.
Katika tukio jingine ,Bakari Saidi (45)mkazi wa Kimanzichana Kusini ,wilayani Mkuranga, ameuwawa kwa kupigwa risasi kifuani upande wa kulia na kutokea chini ya bega la kushoto ,mgongoni na watu wasiofahamika.
Katika tukio hilo,Omar Ally (55)ambae ni afisa mtendaji wa kijiji cha Kimanzichana Kusini,alijeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye mkono wake wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo kwa matibabu.
Kadhalika katika eneo la tukio kumekutwa maganda mawili ya risasi yanayotumika kwenye silaha ya SAR/SMG .
Kamanda Mushongi alisema watu hao walivamia katika ofisi ya serikali ya kijiji cha Kimanzichana Kusini na kufanya mauaji hayo ambapo mtu huyo alifariki dunia na mwingine mmoja kujeruhiwa.
Anasema tukio hilo limetokea octa 5 mwaka huu,majira ya saa 11 alifajiri katika kitongoji cha Ukwama kata ya Kimanzichana tarafa ya Mkamba wilayani hapo.
“Wakati marehemu akiwa najaza fomu za mkopo wa akiba ya Commerce bank(ACB)ghafla walitokea watu wawili wakiwa na silaha mbili na kuanza kuwafatulia risasi na kutoweka kusikojulika wakitumia usafiri wa pikipiki”alisema kamanda Mushongi.

Kamanda huyo alifafanua kuwa mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga na utakabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi mara baada ya uchunguzi kukamilika.
Jeshi hilo liimewahakikishia wananachi wote usalama wao na kwamba linapambana kwa nguvu na wale wenye nia ya kuwatia hofu wananchi,kwani hawataweza kufanikiwa katika mipango yao walijiwekea.

Limewaasa wananchi kuwafichua wahalifu ambao ni sehemu za jamii wanapoishi badala ya kuoneana muhali pamoja na kutoa taarifa pale wanapobaini kuna watu ama raia asiyemwema/waaalifu.

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : MWALIMU WA MADRASA ADAIWA KUHUSIKA NA MAFUNZO YA KIGAIDI
MWALIMU WA MADRASA ADAIWA KUHUSIKA NA MAFUNZO YA KIGAIDI
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2016/10/MUSH.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/mwalimu-wa-madrasa-adaiwa-kuhusika-na.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/10/mwalimu-wa-madrasa-adaiwa-kuhusika-na.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy