Mke wa msanii wa muziki Dogo Janja, Irene Uwoya ametoa majibu juu ya habari zilizopo za mumuwe kutaka kuongeza mke wa pili hadi wann...
Mke wa msanii wa muziki Dogo Janja, Irene Uwoya ametoa majibu juu ya habari zilizopo za mumuwe kutaka kuongeza mke wa pili hadi wanne.
Uwoya ametoa majibu hayo baada ya kukuta habari zimezagaa
katika mitandao mbalimbali juu ya mpingo ya mumuwe aliyoweka ya kutaka
kufikisha idadi ya wake wanne katika ndoa.
“Ndoutajua mim Kabila gani…thubutu uwone tena
wasikudanganye @dogojanjatz,” ameandika mrembo huyo katika mtandao wake
wa kijamii wa Instagram mapema leo baada ya kuona stori za mumuewe za
kumuongezea mke zikitawala.
Katika kipindi cha The Playlist ya Times Fm kilichoruka
juzi ( 12-03-2018) mkali huyo wa ‘Wayu Wayu’ alidai kuwa anampango wa
kuongeza mke wa pili hadi wanne kila baada ya miaka 10.