Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru, anawatangazia watanzania wote wenye sifa na uwezo, kuomba kazi ya Afisa M...
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Arusha wilaya ya Arumeru, anawatangazia watanzania wote wenye sifa na uwezo, kuomba kazi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji Daraja la III katika Halmshauri yake, kwa masharti ya ajira ya kudumu.
Tangazo limetolewa baada ya kupokea kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. Na.CFC 26/205/01 "FF" cha tarehe 22/08/2017, pamoja na barua ya nyongeza ya muda wa utekelezaji wa kibali cha ajira mbadala kwa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa cheny Kumb. Na. CFC 26/205/01 "GG"/95 cha terehe 12/03/2018.
Vibali hivi vimetoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.
Mkurugenzi anawataka watanzania wote wenye sifa kuchangamkia fursa hiyo.Mwisho wa kutuma ombi hilo ni tarehe 03/04/2018.
Bofya kwa maelezo zaidi........TANGAZO LA KAZI.pdf