http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

ANGALIA MFANYABIASHARA AUAWA KINYAMA, ATUPWA KISIMANI


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

WIMBI la kuuawa na kisha miili kutupwa kwenye vi­sima vya maji wilayani Bu­tiama limezidi kuongezeka baada ya mfanyabiashara mmoja, mka...

BIBI HARUSI AJARIBU KUMUUA MUME WAKE SAA CHACHE BAADA YA KUFUNGA NDOA
Diamond Kampeleka Zari Mombasa na Kuwachamba Wanaomsema Vibaya
Mtangazaji wa Azam Tv Katoweka kwenye mazingira ya kutatanisha
WIMBI la kuuawa na kisha miili kutupwa kwenye vi­sima vya maji wilayani Bu­tiama limezidi kuongezeka baada ya mfanyabiashara mmoja, mkazi wa Kijiji cha Busirime, kata ya Butuguri wilayani Butiama mkoani Mara, Charles Magesa (31) kukutwa mwili wake ukiwa unaelea ndani ya maji katika kisima kilichopo kando ya nyumba moja ya kulala wageni iliyopo katika Kijiji cha Isaba kata ya Buruma, Butiama.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo la kusikitisha, baba mzazi wa Charles, Alphonce Magesa, alisema kijana wake aliondoka nyumbani Machi 20, mwaka huu, majira ya saa 2.00 usiku na kwenda Isaba Senta akiwa katika matembezi yake ya kawaida ya kila siku.
Mzee Magesa alidai kuwa, kijana huyo hakurudi siku hiyo nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yake na kesho yake ndipo alipopata taarifa kuwa kijana huyo siku hiyo, majira ya saa 7.00 usiku akiwa kwenye baa moja hapo Isaba, ali­vamiwa na kundi la watu wanne na kuanza kupigana nao.
Baba huyo alifafanua kwamba, baada ya kupata taarifa hizo za kijana wake kuonekana akipigana na kwa kuwa alikuwa hajaonekana nyumbani, aliingiwa na hofu akaichukua familia yake na kuanza kumtafuta maeneo tofauti kijijini hapo bila mafanikio.
Alieleza kuwa, alfajiri ya Machi 22, walimtafuta hasa jirani na eneo alilokuwa akipigana na walipofika karibu na nyumba moja ya kulala wageni ambayo haina jina ambayo pia ina baa ambayo Charles na hao watu walikuwa wakipata vinywaji, walishtuka kukuta mwili wa mpendwa wao ukielea ndani ya maji kisimani huku upande mmoja wa sehemu ya kichwa ukiwa na jeraha kubwa linaloashiria kuwa marehe­mu alipigwa kwenye ugomvi huo na kitu kizito hadi kupoteza uhai.
Tukio hilo ni la pili kutokea wilayani Bu­tiama kwa kipindi cha wiki moja, ambapo katika tukio la kwanza lililotokea Machi 13, mwaka huu, mwili wa mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyakiswa, Kata ya Kyanyari, Jerald Manyama (44) ulikutwa pia ukielea ndani ya maji kisimani kijijini hapo am­bapo pia ilidaiwa kuwa naye alionekana akiwa baa kabla ya kukutwa na mauti.
Charles Magesa enzi za uhai wake.
Polisi wilayani Butiama wamethibiti­sha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia mkazi mmoja wa Kijiji cha Isaba, miongoni mwa watuhumiwa wanne wanaosadikiwa kutekeleza mauaji hayo ambao walionekana wakipigana na marehemu kwenye baa hiyo.
Polisi wamesema chanzo cha ugomvi uliosababisha kuuawa kwa Charles bado hakijafahamika, uchunguzi unaendelea.Marehemu Charles alizikwa Machi 22, mwaka huu kijijini kwao, Busirime na ameacha mtoto mmoja.
Stori: GREGORY NYANKAIRA, Mara

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : ANGALIA MFANYABIASHARA AUAWA KINYAMA, ATUPWA KISIMANI
ANGALIA MFANYABIASHARA AUAWA KINYAMA, ATUPWA KISIMANI
https://matukiotz.co.tz/wp-content/uploads/2018/03/MAJIII-768x432-678x381.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/angalia-mfanyabiashara-auawa-kinyama.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/03/angalia-mfanyabiashara-auawa-kinyama.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy