Kijana aliyefahamika kwa majina ya Joseph Medardi (32) mkazi wa Nyakahanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amemuuwa mama mkwe wake...
Kijana aliyefahamika kwa majina ya Joseph Medardi (32) mkazi wa
Nyakahanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amemuuwa mama mkwe wake
Elizabeth Simon (70) kwa kumkata kata mapanga na kumjeruhi mkewe Elice
Joseph (28) kisha na yeye kujimwagia petroleum.
Kijana
huyo amefanya tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na
matatizo na mkewe kuhusu suala la unyumba jambo ambalo lilimpelekea
kumrudisha mkewe huyo nyumbani kwa mama yake, ambapo amekaa huko
takribani wiki tatu, siku moja kabla ya kikao cha kuwasuluhisha wanandoa
hao ndipo kijana huyo ametekeleza mauaji hayo.
Mtoto wa marehemu Elizabeth Simon (70) ambaye ni Mchungaji Ezekia Simon amesimulia jambo hilo kwa undani zaidi na kusema kuwa chanzo cha yote hayo kuwa ni matatizo ya unyumba na kudai kuwa kijana huyo ambaye yeye ni shemeji yake alionekana amekuja na kusudio la kuwauwa wote yaani mama yake pamoja na mdogo wake huyo ambaye amejeruhiwa tu.
"Kisa cha kifo cha mama kimetokana na Mume wa dada kutoelewana katika habari za unyumba walikuwa na mgogoro kwa maana hiyo ikapelekea kumfukuza mkewe hivyo alikuja hapa yapata kama takribani wiki tatu yuko hapa nyumbani na baada ya hapo mimi kama Mkuu wa familia nilijaribu kutafuta njia ya kuwasuluhisha hivyo tarehe ambayo tulipanga kukutana ilikuwa jana ingawa hatukufanikiwa kukutana baada ya mzazi wa kijana kusema hakupata taarifa, matokeo yake yule kijana ndiyo amekuja akawashambulia mama pamoja na dada na kusababisha mauti ya mama"
Mchungaji Simon aliendelea kusimulia jambo hilo
"Yule kijana alikuja kwa lengo la kuuwa wale na yeye kujiuwa kwa sababu alipowashambulia na kuwajeruhi yeye alijimwagia Petroleum na kujichoma moto ndani ya nyumba hii hii"