Fredy Swai na Mama Kanumba. KUTOKANA na hivi karibuni mama wa aliyekuwa staa mkubwa wa filamu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumwanika ...
| Fredy Swai na Mama Kanumba. |
KUTOKANA na hivi karibuni mama wa aliyekuwa staa mkubwa wa filamu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa kumwanika kijana ambaye ni mwigizaji wa tamthilia, Fredy Swai kuwa ndiye mrithi wa mwanaye, kijana huyo alibadilika muonekano usoni baada ya wanahabari kumhoji kuhusu ukaribu wake na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye alikuwa mpenzi wa Kanumba.
Fredy aliulizwa kama anamawasiliano na Lulu, alikosa jibu la moja kwa moja na alijibu tofuti na maswali aliohojiwa mwanzo, kwa hali ya kujilazimisha alijibu kuwa hana namba ya Lulu huku akionesha hali ya kukosa amani.
' Lulu'
Bado haijafahamika kwanini alitahamaki vile kiasi cha kushindwa kujibu ndiyo ndio ua hapana na badala yake akakausha kwanza, baadaye akaanza kutoa maelezo.
Akizungumza na wanahabari, Fredy alisema hana namba ya Lulu na hajawahi kukutana na Lulu na endapo atakutana nae ataongelea kazi tu kwani amekuwa akizifuatilia sana kazi zake na si vinginevyo.
Credity.................................Global Publishers



