http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu UCHI....Tazama Majina ya Baadhi Yao waliofungiwa kazi zao


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa, serikali inafuatilia kwa karibu wasanii wote wanaoweka ...

Taarifa Kwa Umma Kutoka Wizara Ya Afya Kuhusu Uvumi Unaosambazwa Katika Mitandao ya Kijamii
Sitta ahamishwa nyumba ya Serikali.....Awamu ya tano yagoma kumlipia kodi ya pango, Ahamia Mtaa wa Manzese
Marekani kuongeza wanajeshi Sudan Kusini
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema kuwa, serikali inafuatilia kwa karibu wasanii wote wanaoweka picha za kukosa maadili kwenye mitandao na kuwachukulia hatua.

Shonza ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaama alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari. Agizo hilo la Naibu Waziri ni matokeo ya kauli iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli aliyoitoa mjini Dodoma wakati akizungumza na Jumuiya ya Wazazi ya CCM. 

Rais Magufuli alivitaka vyombo husika kuwachukulia hatua wasanii hasa wa kike ambao wamekuwa wakivaa nguo zinazopelekea kumomonyoka kwa maadili.

Wakati akizungumza hayo Naibu Waziri alitaja majina ya wasanii ambao wameanza kuwachukulia hatua ambapo baadhi wametakiwa kufika ofisini kwake huku mwingine akifungiwa kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda wa miezi sita.

Shonza amemtaka msanii, Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi kufika ofisini kwake mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na maadili.

Mbali na Sanchi, Shonza ametoa maagizo, ”Ninamtaka Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufika ofisini kwangu mara moja sababu alitumiwa ujumbe lakini hakujibu, hivyo ajue kuwa hawezi kushindana na serikali.”

Pia, Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza amemfungia msanii wa filamu na muziki, Suzan Michael maarufu Pretty Kind kujihusisha na shughuli zote za sanaa kwa muda wa miezi sita, kutokana na kuweka picha za utupu katika mtandao ya kijamii.

Wakati huo huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amewasisitiza wamiliki wa studio za kutayarisha kazi za sanaa na waandaji wa kazi za sanaa (Producers) kujisajili katika ofisi za Baraza hilo. Asisitiza, kufanya kazi bila kusajiliwa ni kinyume na sheria.


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu UCHI....Tazama Majina ya Baadhi Yao waliofungiwa kazi zao
Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu UCHI....Tazama Majina ya Baadhi Yao waliofungiwa kazi zao
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyCEq677NtxpYtm9W0ARyHNB3XVDmeQWlQcvomxaIj8_UDtmB3Cs6CoYQ8RuS577NEpJOBDideOD9FwagDvHCUx6cMujryrVMbiMckpyf4Sj4LnJq3A4IGUPwNyGc-qa-MJ75j5jYRfMQq/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyCEq677NtxpYtm9W0ARyHNB3XVDmeQWlQcvomxaIj8_UDtmB3Cs6CoYQ8RuS577NEpJOBDideOD9FwagDvHCUx6cMujryrVMbiMckpyf4Sj4LnJq3A4IGUPwNyGc-qa-MJ75j5jYRfMQq/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2018/01/serikali-yaanza-kuwashughulikia-wasanii.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2018/01/serikali-yaanza-kuwashughulikia-wasanii.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy