http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Marekani kuongeza wanajeshi Sudan Kusini

Image caption Mapigano yalisitishwa Jumatatu usiku mjini Juba Marekani imesema itawatuma wanajeshi 40 zaidi Sudan Kusini kusaidia kulind...


Mapigano
Image captionMapigano yalisitishwa Jumatatu usiku mjini Juba
Marekani imesema itawatuma wanajeshi 40 zaidi Sudan Kusini kusaidia kulinda Wamarekani na mali ya Marekani mjini Juba.
Msemaji wa jeshi la Marekani barani Afrika, Africom, Jennifer Dyrcz amesema wanajeshi hao wa Marekani wametumwa nchini humo baada ya mapigano yaliyoanza wiki iliyopita.
Kwa sasa hali imetulia baada ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Rais Riek Machar kuagiza wanajeshi wao wasitishe vita Jumatatu.
Ubalozi wa Marekani mjini Juba, kwa mujibu wa shirika la habari la AP, umesema raia wa Marekani wanaotaka kuondoka Sudan Kusini watasaidiwa kuondoka kwa ndege.
Wafanyakazi wasio muhimu sana katika ubalozi huo pia wataondolewa.
Mashirika makubwa ya ndege yalisitisha safari za ndege kutua na kupaa kutoka Juba.
Safari za ndege za kibinafsi na za kukodisha hata hivyo zimerejelewa na ndege hizo zinatumiwa kuwaondoa wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada pamoja na raia wa kigeni kutoka Juba.
Umoja wa Mataifa umesema raia 36,000 wa Sudan Kusini wametoroka makwao kutokana na mapigano na kutafuta hifadhi makanisani, katika kambi za UN na kambi za mashirika ya kutoa misaada.
Image copyrightAFP
Taarifa zinasema serikali ya India pia imefanya mipango ya kuwaondoa raia wake kutoka nchini humo kwa kutumia ndege Julai 14.
"Safari zaidi zitapangwa baadaye kukiwepo na hitaji,” tovuti ya habari ya Tamazuj imesema, ikunukuu taarifa kutoka ubalozi wa India nchini Sudan Kusini.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Marekani kuongeza wanajeshi Sudan Kusini
Marekani kuongeza wanajeshi Sudan Kusini
http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2016/06/28/160628144718_south_sudan_war_640x360_bbc_nocredit.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/marekani-kuongeza-wanajeshi-sudan-kusini.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/marekani-kuongeza-wanajeshi-sudan-kusini.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy