http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Nyalandu aikimbia CCM , aomba kujiunga CHADEMA


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Lazaro Nyalandu amejiuzulu nafasi yake ndani ya CCM na kujiuzulu nafasi...

JPM: Sitoi Chakula cha Msaada Ng’o, Asiyefanya Kazi Asile, Asiyekula Afe!
Zaidi ya gunia 400 za Bangi zakamatwa na kuteketezwa kwa moto.
Wafanyabiashara wa Mafuta ya Petrol na Dezel Dodoma Wapewa Siku 10

Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Lazaro Nyalandu amejiuzulu nafasi yake ndani ya CCM na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia CCM kwa kile alichodai hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Nyalandu ameandika Ujumbe huu kama unavyosomeka.
”Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
Halikadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Job Ndugai, barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
Aidha, Nimechukua uamuziI huo kutokana na kutoridhishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya Mihimili ya dola Serikali, Bunge, na Mahakama kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana Kikatiba.
Vilevile, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
Mimi Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,  kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. Aidha, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Hivyo basi, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya Kikatiba, natangaza Kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba Ikiwapendeza wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia Malangoni mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
Vilevile, nimemua kujiuzulu Kiti Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa Uchaguzi mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua Itikadi wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, Sote kama Taifa tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa Mungu kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano  wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na Taifa lililo imara na nchi yenye maadili” ameandika Nyalandu.


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Nyalandu aikimbia CCM , aomba kujiunga CHADEMA
Nyalandu aikimbia CCM , aomba kujiunga CHADEMA
https://i2.wp.com/dar24.com/wp-content/uploads/2017/10/nyala.jpg?resize=960%2C636
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/10/nyalandu-aikimbia-ccm-aomba-kujiunga.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/10/nyalandu-aikimbia-ccm-aomba-kujiunga.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy