http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

MSANII CHID BENZ AKAMATWA TENA NA DAWA ZA KULEVYA


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, limewakamata watu saba akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ ...

Video: Alikiba atua Afrika Kusini kuanza ziara yake
Video Mpya : Diamond Platnumz f/ Ne-Yo – Marry You
Umeisikia Hii ya Vanessa Mdee,Afunguka Siri ya Mafanikio Yake..!!!

Jeshi la polisi Mkoa wa Ilala, limewakamata watu saba akiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro maarufu kama ‘Chid Benz’ kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 12 mwaka huu saa 11.50 jioni wakijihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

Amesema jeshi la polisi limefanya msako wake na kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo ambalo linajihusisha na uuzaji wa dawa hizo.

“Chid Benz na wenzake wapo kituo cha Polisi cha msimbazi ambapo tunaendelea na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani na kiasi cha dawa zilizokamatwa zimepelekwa kwa mkemia mkuu na itajulikana ni kiasi gani za dawa za kulevya zilizokamatwa,”amesema Hamduni.

Hamduni amesema jeshi hilo linafanya msako liweze kubaini mtandao mzima unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na watumiaji ili kuhakikisha wote wanachukuliwa hatua na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Itakumbukwa kuwa , Oktoba 24,2014, Chid alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNIA) jiji la Dar es Salaam akiwa na dawa za kulevya, akijaribu kuvuka nazo kwenda mkoani Mbeya kushiriki onyesho la Instagram Party wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria .

Msanii huyo wa kizazi kipya alikiri shtaka hilo na ndipo , Februari 26 mwaka 2015, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipomhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh900,000 baada ya kupatikana na hatia ya katika makosa matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi na Heroine yenye thamani ya Sh 40,358.


Hata hivyo msanii huyo alifanikiwa kulipa faini na kukwepa kifungo hicho.


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : MSANII CHID BENZ AKAMATWA TENA NA DAWA ZA KULEVYA
MSANII CHID BENZ AKAMATWA TENA NA DAWA ZA KULEVYA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhh2TCZn47seKdWUZrjw96CgdzRsba3yXsUJsVImgOFFojAvlvk9_4rc8C5z_8T-5MxAIvowEbLdhfOKp6i_NJjL09RBfJ-41YMt7NTANWyLVuJU3nA8TnoXqjgAr43gnsQkMj6C-i_WOzc/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhh2TCZn47seKdWUZrjw96CgdzRsba3yXsUJsVImgOFFojAvlvk9_4rc8C5z_8T-5MxAIvowEbLdhfOKp6i_NJjL09RBfJ-41YMt7NTANWyLVuJU3nA8TnoXqjgAr43gnsQkMj6C-i_WOzc/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/msanii-chid-benz-akamatwa-tena-na-dawa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/08/msanii-chid-benz-akamatwa-tena-na-dawa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy