http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Moto waua na kujeruhi


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mtu mmoja (75) amefariki katika ajali ya moto huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya (wote wa familia moja) huko Lumumba Wilaya...

Breaking News: Zitto Kabwe alala Mahabusu na aachiwa kwa dhamana ya mil.50
Mwanamke amuua mumewe kwa shoka naye kujinyonga
FUATILIA IBADA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU AKWILINA




Mtu mmoja (75) amefariki katika ajali ya moto huku wengine wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya (wote wa familia moja) huko Lumumba Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza siku ya Ijumaa, ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.

Tukio hilo limetokea ya majira 12:30 jioni mtaa wa Lumumba ambapo inadaiwa kwamba kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu alikua ndani ya nyumba yake pamoja na watoto wake, ndipo ghafla ulizuka moto mkali uliokuwa unaunguza nyumba yake, na kwamba kutokana na taharuki marehemu alianza kukusanya mali zake ndani ili aweze kutoka nazo nje ndipo kwa bahati mbaya moto ulimzidia na yeye kushindwa kutoka nje na kupelekea kuungua zaidi na baadae kufariki dunia.

Hata hivyo inasemekana kwamba kutokana na miundombinu mibovu ndiyo iliyopelekea kukosa haraka msaada wa zimamoto ambapo ukuta uliopo jirani na maeneo hayo ulipelekea gari la wanajeshi wa zimamoto pamoja na jeshi la polisi kufika eneo la tukio kwa kuchelewa na kushindwa kuokoa maisha ya mfanyabiashara Maduhu Masunga, ingawa waliweza kudhibiti moto usiharibu maeneo mengine ya jirani.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Ahmed Msangi anatoa pole kwa wanafamilia wa marehemu, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba akini pia anawaombea majeruhi wapone haraka na kuwataka wanafamilia waendele kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo mwili wa marehemu bado unafanyiwa uchunguzi, na kuwaasa wananchi kujitahidi kuweka vizuri miundombinu ya umeme.

Aidha thamani ya mali na vitu vilivyoteketea katika ajali hiyo ya moto bado haijafahamika, jeshi la polisi pamoja na jeshi la zima moto kwa kushirikiana na tanesco wanaendelea kufanya uchunguzi na upelelezi kuhusiana na tukio hilo ili kujua chanzo cha moto huo, majeruhi Ngalula Maduhu 39, Brian Maduhu 26, wamepelekwa hospitali ya mkoa ya Sekou Toure kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Moto waua na kujeruhi
Moto waua na kujeruhi
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2017/06/11/Moto%20.jpg?itok=TQzyRYk7×tamp=1497201507
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/moto-waua-na-kujeruhi.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/06/moto-waua-na-kujeruhi.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy