http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mwalimu asimulia safari iliyoua wanafunzi 32


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Wakazi wa Rhotia, wilayani Karatu mkoani Arusha wakitazama basi dogo lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Lu...

Bunge la Afrika Kusini limeshindwa tena kumuondoa Rais Zuma
MGOMBEA URAIS RAILA ODINGA APINGA MATOKEO YA UCHAGUZI YANAYOTANGAZWA NA TUME YA UCHAGUZI IEBC
Mtumbwi Wazama na Kuua Watatu


Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Lucky Vicent Academy waliyokuwa wanasoma wanafunzi 32 waliofariki dunia kwa ajali jana, Longino Vicent amesema ndiye aliyesimamia safari iliyosababisha vifo vya watoto hao na wafanyakazi watatu.

Vicent amesema wanafunzi hao na walimu wawili pamoja na dereva waliofariki, walianza safari yao saa 12:30 asubuhi kuelekea Karatu ambako watoto hao walipaswa kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wale wa Shule ya Tumaini.

“Mimi ndiye niliyesimamia safari hiyo na niliwasafirisha waliondoka hapa saa 12; 30 asubuhi, sikufikiri kama yatatokea haya. Kila kitu kilikuwa salama tu,” alisema akisimulia walivyoanza safari watoto hao kabla ya gari walilopanda aina ya Toyota Costa lenye namba za usajili T 871 BYS kupinduka korongoni na kusababisha vifo hivyo.

Mwalimu Longino alisema shule hizo mbili zimekuwa na tabia ya kufanya mitihani ya ujirani mwema na kuwa hiyo ni mara ya tatu.
“Huu ni mwaka wa tatu, hata shule ya Tumaini huwa inakuja Arusha,” alisema.

Mwalimu huyo alisema shule hiyo ilikuwa ya kwanza kimkoa mwaka 2004 na ya 20 kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
Wanafunzi hao waliofariki dunia walikuwa wakisoma shule hiyo ya bweni ambayo kwa mujibu wa wakazi wa Arusha ni miongoni mwa shule bora na iliyotoa mwanafunzi bora katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga alisema eneo la ajali lina kona nyingi na mteremko mkali na kwamba, kuna maeneo ambayo yamekuwa yakisababisha ajali kutokana na miundombinu yake ilivyokaa.

Aliyataja eneo jingine kuwa lipo barabara ya Morogoro kwenda Dodoma linaloitwa Makunganya lina utelezi mwingi na kuwasihi madereva kuwa makini sana wakati wa mvua. Wanafunzi waliofariki ni wa darasa la saba.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro amesema miili ya wanafunzi hao itaagwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid leo.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mwalimu asimulia safari iliyoua wanafunzi 32
Mwalimu asimulia safari iliyoua wanafunzi 32
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3916934/highRes/1634926/-/maxw/600/-/5wqwd9/-/pic+mwalimu+asimulia+ajali.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/05/mwalimu-asimulia-safari-iliyoua.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/05/mwalimu-asimulia-safari-iliyoua.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy