http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Freeman Mbowe na Tundu Lissu Waitwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu wameandikiwa barua na Sekretarieti ya Maadili ya Viongoz...

GAMBO Awataka waliokula pesa zauma kufunguliwa mashtaka
TRA Yakamata Mali za Lugumi
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro ameendelea na ziara yake ya mafunzo mjini Belgium

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu wameandikiwa barua na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, wakitakiwa kujieleza kwa matamko yao waliyoyatoa katika siku za hivi karibuni.

Lissu amekiri kupokea barua kutoka kwenye Sekretarieti hiyo akieleza kuwa imeandikwa na Jaji mmoja mstaafu ambaye hata hivyo hakumtaja jina.

“Ni kweli mimi na Mwenyekiti Mbowe tumepata barua hiyo. Ni barua ya ajabu ambayo imeandikwa na mtu aliyewahi kuwa Jaji wa mahakama kuu,” Lissu anakaririwa na Mwananchi. “Sitaki kuzungumza mengi kwa sasa, Jumatano nitalizumzia vizuri jambo hili,” aliongeza.

Hata hivyo, Kamishna wa Sekretarieti, Jaji Mstaafu Salome Kaganda alieleza kutofahamu chochote kuhusu barua hiyo iliyodaiwa kuwafikia viongozi hao wa Chadema.

“Mimi sifahamu kuhusu suala hilo, sina taarifa,” Jaji Kaganda alimueleza mwandishi wa gazeti hilo.

Hata hivyo, hali hiyo imeibua maswali kwani viongozi hao wa siasa ambao pia ni wabunge, hawana sifa za kuwa watumishi wa umma na hakuna kiapo cha utumishi wa umma kinachowabana.

Mbowe na Lissu walihojiwa hivi karibuni na Jeshi la Polisi kutokana na matamshi yao wakati wa kutangaza Operesheni UKUTA. Lissu anadaiwa kutoa kauli za kichochezi na kuidharau mahakama.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Freeman Mbowe na Tundu Lissu Waitwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
Freeman Mbowe na Tundu Lissu Waitwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj38YMn9Tb-WI6VDh7VCxBQjdvpacmFUccJj38heBvwAqKG9usP9CAGHt9yUeljcOF-n_Ve3-SB537619V1Fh4nU-SZ6QtIM1ey2tYIaUYEFdmZz2yTA5H4fLhrkzmNNRo7rBXqsen0mcU/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj38YMn9Tb-WI6VDh7VCxBQjdvpacmFUccJj38heBvwAqKG9usP9CAGHt9yUeljcOF-n_Ve3-SB537619V1Fh4nU-SZ6QtIM1ey2tYIaUYEFdmZz2yTA5H4fLhrkzmNNRo7rBXqsen0mcU/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/freeman-mbowe-na-tundu-lissu-waitwa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/08/freeman-mbowe-na-tundu-lissu-waitwa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy