http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mvutano wa CCM na CHADEMA Walitikisa Jeshi la Polisi.........BAVICHA Yaandaa Zaidi ya Vijana 5000 Kuzuia Mkutano, Polisi Mara Yasema Wanacheza Ngoma ya Kitoto


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mvutano wa kisiasa baina ya vijana wa CCM na CHADEMA  kuhusu katazo la mikutano ya vyama vya siasa umezidi kukua huku jeshi la polisi li...

WATOTO WENYE UALBINO WAPAKWA RANGI NYEUSI KUWAKINGA
KIKWETE; KAMA HUJUI KAA KIMYA
Arusha.Mwili wa mtoto waokotwa mferejini


Mvutano wa kisiasa baina ya vijana wa CCM na CHADEMA  kuhusu katazo la mikutano ya vyama vya siasa umezidi kukua huku jeshi la polisi likitarajiwa kutoa tamko kuhusu hali hiyo.

Hali hiyo ya jino kwa jino imejitokeza  zikiwa zimebakia siku 16 kabla ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa CCM July 23, ambao Baraza la Vijana la CHADEMA ( BAVICHA )  limesema litawasaidia polisi kuuzuia.

Tayari BAVICHA limetangaza kuandaa vijana 5000 kutoka sehemu mbalimbali nchini kwenda kuzuia mkutano huo utakaotumika kumkabidhi Rais John Magufuli uenyekiti wa chama hicho.

Jumatatu iliyopita, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka aliionya Bavicha wasiende Dodoma kuzuia mkutano wa CCM kwa kuwa watatumia kila mbinu kuwazuia ili kulinda heshima ya chama chao. 

Shaka alisema mkutano huo utafanyika kama ulivyopangwa, hivyo Bavicha kama kweli ni vidume wa mbegu wajitokeze ili wakione cha mtema kuni. 

Shaka alisema UVCCM wako tayari kuidhihirishia dunia kwa kuwatia adabu Bavicha na kuonya wasijaribu kufanya jambo lolote linalotishia kuhatarisha usalama au ustawi wa maendeleo ya kisiasa ya CCM kwa saa, siku, wakati na mahali popote. 

Shaka aliwataka Bavicha kuacha siasa za mikwara, vitisho, kutishia usalama na amani ya nchi kwa kujifanya vijogoo wakati hawana lolote wanaloweza ama kuzuia, kujenga au kubomoa. 

Alipoulizwa kuhusu mvutano huo, Msemaji wa Polisi nchini, Advera Bulimba alisema jeshi hilo litatoa taarifa na ufafanuzi kuhusu zuio la mikusanyiko ya vyama vya siasa leo. 

Sintofahamu ilivyoanza 
Utata huo uliibuliwa na amri ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi Makao, Nsato Mssanzya ya kuzuia mikutano na maandamano yote ya vyama kwa madai kwamba vyanzo vyake vya kiintelejensia vilibaini kuwapo kwa uwezekano wa kutokea kwa vurugu. 

“Jeshi la polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara kuanzia Juni 7, mwaka huu hadi hapo hali ya usalama itakapotengamaa." Ilisema sehemu ya taarifa ya jeshi la polisi


Baada ya katazo hilo, jeshi hilo lilitawanya mikutano ya ndani ya Chadema, yakiwamo mahafali ya vijana wa chama hicho (Chaso) yaliyopangwa kufanyika Dodoma kwa madai ya kuwapo mlipuko wa ugonjwa usiofahamika. 

Hatua hiyo ya polisi ilikuja baada ya Chadema kutangaza mpango wa kuzunguka nzima kueleza masaibu ya kidemokrasia yanayokikumba na baadaye CCM kutangaza kupita katika maeneo hayo ‘kufuta nyayo”.

Katibu wa Bavicha, Julius Mwita alisema mpaka jana tayari vijana 5,000 walikuwa wakijiandaa kwenda Dodoma; “kushirikiana na polisi kuwafundisha CCM kuheshimu amri zinazotolewa na viongozi. "

"Tumeandaa vijana 5,000 kutoka mikoa 19 nchini ambao wamejitolea kwa nauli zao kwenda Dodoma kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha mkutano wa CCM haufanyiki.” 

Watembelea Butiama 
Katika hatua nyingine, viongozi wa Chadema juzi walitembelea kaburi  la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere huko Butiama, wakisema walikwenda kumshtaki Rais Magufuli kwa kuminya demokrasia. 

Mwenyekiti wa Bavicha, Pastrobas Katambi alisema chama hicho kinatambua jitihada zilizofanywa na Mwalimu Nyerere katika kukuza na kuendeleza ustawi wa jamii ya kidemokrasia nchini.

“Tunapenda kuwaambia watawala kwamba amani ni tunda la haki na ni muhimu utawala ukaheshimu misingi ya kikatiba iliyoachwa na Baba wa Taifa,” alisema Katambi. 

Kauli za CCM, Chadema 
Naibu Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika alisema anabariki maandalizi ya mpango na kitendo kinachotarajiwa kufanywa na Bavicha ili kuwepo na usawa wa kidemokrasia. 

“Kama ni ruhusa iwe kwa wote na kama zuio liwe kwa wote, haina maana Chadema wazuiwe lakini CCM waendelee na mikutano yao ya kisiasa,” alisema Mnyika. 

Kaimu Katibu wa CCM, Mkoa wa Dodoma alisema mkutano huo ni wa kitaifa na wala si wa mkoa na kushauri atafutwe Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka. 

“Sisi tunatekeleza maagizo tunayopewa na si vinginevyo,” alisema. Ole Sendeka hakupatikana na simu yake ilikuwa inaita bila kupokelewa. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema mkutano wa CCM ni wa ndani wala hakuna tatizo lolote kwa kuwa mikutano ya ndani inaruhusiwa na kuwa jeshi hilo litawalinda wanaCCM. 

Kuhusu Jeshi hilo kuzuia mikutano ya Chadema, Mambosasa alisema walizuia bendera na si vinginevyo na kuwa alitoa taarifa ikiwa kamili lakini waandishi walipotosha. 

Manyara wajiandaa
Zaidi ya vijana 560 wa Mkoa wa Manyara, wamejiandikisha tayari kuelekea Dodoma kwa ajili ya kuwasaidia polisi kuzuia mkutano wa CCM ili kuunga mkono agizo la kupigwa marufuku mikusanyiko ya kisiasa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Francis Massawe aliwataka vijana hao kuachana na mpango huo wa kitoto kwani wao wamejipanga kushughulika na watu wanaotaka kuanzisha vurugu. 

Kamanda Massawe alisema endapo kuna kundi linataka kukwamisha mkutano halali wa CCM wa kumchagua mwenyekiti wao, wasubiri hadi mwaka 2020 ndipo wafanye na kwamba polisi hawatakubali hilo litokee. 

“Hao vijana wanacheza ngoma ya kitoto ambayo haikeshi kwani wanaingilia majukumu ambayo siyo yao, uchaguzi wa CCM hauna ubishi lazima ufanyike na hakuna wa kuzuia, hao wanacheza kombolela,” alisema. 

Msimamo wa Zitto
Akizungumzia uamuzi wa Bavicha, Kiongozi wa ACT Wazalendo ambacho pia mitano yake imezuiwa, Zitto Kabwe alisema haoni tatizo kuhusu suala hilo kwa kuwa wanafanya siasa, hivyo haoni kama ni njia mbaya.

Zitto alisema chama chake hakiwezi kusema moja kwa moja kuwa kinaunga mkono uamuzi wa Bavicha lakini wao watakwenda mahakamani kupinga hatua ya Serikali kuzuia uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano yao. 

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mvutano wa CCM na CHADEMA Walitikisa Jeshi la Polisi.........BAVICHA Yaandaa Zaidi ya Vijana 5000 Kuzuia Mkutano, Polisi Mara Yasema Wanacheza Ngoma ya Kitoto
Mvutano wa CCM na CHADEMA Walitikisa Jeshi la Polisi.........BAVICHA Yaandaa Zaidi ya Vijana 5000 Kuzuia Mkutano, Polisi Mara Yasema Wanacheza Ngoma ya Kitoto
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHB7vbL4GmPEGVryqDv3DacIhaFl9YXCQQNpBK8-RUjxPH07DuznkpMteyPx7THBqm3HCqxyQbzjg-eZetLJ0GsRBB2yYStH5rjhDmh7ruFf1Io898KZlyvmJQB1oQY81wwEI7tVr8FQQ/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHB7vbL4GmPEGVryqDv3DacIhaFl9YXCQQNpBK8-RUjxPH07DuznkpMteyPx7THBqm3HCqxyQbzjg-eZetLJ0GsRBB2yYStH5rjhDmh7ruFf1Io898KZlyvmJQB1oQY81wwEI7tVr8FQQ/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/mvutano-wa-ccm-na-chadema-walitikisa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/mvutano-wa-ccm-na-chadema-walitikisa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy