Mahakama nchini Ufaransa imetoa hati ya kukamatwa kwa Mfalme wa muziki aina ya Rumba raia wa DRC Koffi Olomide ambaye anadaiwa kushamb...
Mahakama nchini Ufaransa imetoa hati ya kukamatwa kwa
Mfalme wa muziki aina ya Rumba raia wa DRC Koffi Olomide ambaye anadaiwa
kushambulia kingono na kuwapiga wachezaji wake wanne wakiwa Paris kati
ya mwaka 2002 na 2006.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 61 aliondolewa nchini
Ufaransa mwishoni mwa mwezi Januari kufuatia madai ya unyanyasaji
aliyotekeleza nchini Ufaransa.
Wachezaji wake wanne wameeleza kuwa walilazimishwa kufanya
ngono mara kadhaa wakiwa Drc au ziarani huku wakitaja walipokuwa
ufaransa walifungiwa chumbani kwa saa 24 chini ya ulinzi wa wanaume
watatu katika kitongoji kimoja jijini Paris.
Wachezaji hao wameeleza mara kadhaa kulazimishwa kufanya
ngono bila kutumia kinga hotelini lakini pia studio ambapo walipigwa
pale walipokataa.
Kwa mujibu wa walalamika wamedai kufanya matakwa ya
mwanamuziki huyo baada ya kutishiwa kukosa kibarua,madai ambayo
yanadaiwa kusemwa na wachezaji wake wote wakike.



