Thomas Manning anaonekana mwenye furaha baada ya upasuaji Hospitali moja mjini Boston imekuwa ya kwanza nchini Marek...
Hospitali moja mjini Boston imekuwa ya kwanza nchini Marekani kufanya Operesheni ya kupandikiza uume.
Madaktari wamesema zoezi hilo limefanikiwa na kumfanya Manning kuwa mtu wa tatu dunia nzima kufanyiwa upasuaji huo.
Mmoja wa madaktari waliofanya upasuaji huko Boston ni Dicken Ko, amesema wanaume wanaopoteza maungo yao hupata athari za kisaikolojia kwa kuwa ni maeneo nyeti yanayoathirika wengi wao hawapendi kufahamika hadharani.