http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya agoma kujiuzulu

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, Wafura Chebukati ametangaza rasmi kuwa uchaguzi wa rais nchini humo utarudiwa kama ilivyoagizwa...



Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya, Wafura Chebukati ametangaza rasmi kuwa uchaguzi wa rais nchini humo utarudiwa kama ilivyoagizwa na mahakama huku akisisitiza kuwa hatajiuzulu nafasi hiyo.

Akizungumza na wanahabari baada ya mahakama ya juu ya nchi hiyo kuufuta uchaguzi uliofanyika Agosti 8, mwaka huu, Chebukati amesema tume hiyo ndicho chombo pekee chenye mamlaka kikatiba ya kuendesha uchaguzi na si vinginevyo.

Amesema tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mpya ulioamriwa kufanyika ndani ya siku 60, itatangazwa ndani ya siku chache zijazo.

Kuhusu yeye na wenzake katika tume hiyo kuachia ngazi, Chebukati amesema haoni sababu ya kujiuzulu huku akimtaka mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwenda kwenye tume hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wake ili kujiridhisha endapo kulikuwa na ukiukwaji wa sheria kama ilivyoelezwa na mahakama.

Amesisitiza kuwa zoezi la upigaji kura halikuwa na kasoro zozote za kisheria na kusema, "Uamuzi wa mahakama umejikita zaidi kwenye zoezi la kutangaza matokeo na siyo zoezi la upigaji kura,” Licha ya kusisitiza kuwa uchaguzi huo ulifuata sheria, Chebukati amesema atalazimika kuifanyia mabadiliko madogo tume hiyo kutokana na dosari chache zilizobainika wakati wa utoaji wa matokeo

COMMENTS


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya agoma kujiuzulu
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini kenya agoma kujiuzulu
https://dsh7tu7hoh3mx.cloudfront.net//uploads/story/Wafula-Chebukati_1504272751.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/mwenyekiti-wa-tume-ya-uchaguzi-nchini.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/09/mwenyekiti-wa-tume-ya-uchaguzi-nchini.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy