Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato cha sita ...
Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia watuhumiwa
wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanafunzi wa kike wa kidato
cha sita Sundi George aliyekuwa akisoma katika shule ya sekondari
Mwembetogwa.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi
Iringa ACP Juma Bwire amesema mnamo Machi 12 mwaka huu akiwa na sare za
shule mwanafunzi huyo alitoka nyumbani kwao kuelekea shuleni lakini
hakurudi hadi mwili wake ulipopatikana maeneo hayo.
Kamanda Bwire amesema wanaendelea na uchunguzi kubaini
chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo huku akiwaomba wananchi kutoa
taarifa kwa mtu yoyote wanayehi amehusika katika tukio hilo.