http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mamia waandamana kupinga mauaji Kenya

Mamia ya watu wameandamana jijini Nairobi, Kenya kupinga mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na maafisa wa usalama nch...

Mashirika
Mamia ya watu wameandamana jijini Nairobi, Kenya kupinga mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na maafisa wa usalama nchini humo.
Maandamano hayo yamefanyika kufuatia kupatikana kwa miili ya wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri.
Bw Kimani na Bw Mwenda walikuwa wameabiri gari la Bw Muiruri baada ya kuhudhuria kesi katika mahakama ya Mavoko 23 Juni, walipotekwa na watu wanaodaiwa kuwa maafisa wa usalama.
Inadaiwa walizuiliwa kwa muda katika kituo cha polisi wa utawala cha Syokimau.
Miili yao ilipatikana mtoni eneo la Ol Donyo Sabuk, mashariki mwa jiji la Nairobi, ikiwa imefungwa mkono na ikionekana kuwa na ishara za majeraha.

"Mauaji ya vijana hawa watatu yanafaa kumtia wasiwasi Rais Kenyatta," amesema Bw George Kegoro, mkurugenzi mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Tume ya Haki za Binadamu Kenya.
"Kiongozi wa nchi ni sharti aunde jopo la uchunguzi kuhusu kutekwa na kutumiwa vibayakwa idara za polisi na rasilimali zake kwa manufaa ya watu binafsi na katika kutekeleza uhalifu ikiwa ni pamoja na, katika kisa hiki, mauaji ya kiholela."

Chama cha Wanasheria Kenya (LSK) kimewashauri wanachama wake kususia shughuli za mahakama kulalamikia kuuawa kwa wakili mwenzao, Bw Kimani.
Waandamanaji wameanzia msafara wao eneo la Freedom Corner, uwanja wa Uhuru Park na kupitia katikati mwa jiji ambapo watafika pia makao makuu ya polisi na makao makuu ya idara ya mahakama.
Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wanataka Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet na Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery wajiuzulu.
Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia visa vya ukatili wa polisi dhidi ya raia Kenya la IMLU, mwaka 2015 watu 125 waliuawa kiholela na maafisa wa polisi.
Kati ya Januari na Aprili mwaka huu, watu 53 tayari wameuawa kwa mujibu wa IMLU.
Maafisa watatu wa polisi waliotuhumiwa kuhusika katika kutoweka kwa Bw Kimani, Bw Mwenda na Bw Muiruri wamekuwa wakizuiliwa na walitarajiwa kufikishwa kortini leo.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mamia waandamana kupinga mauaji Kenya
Mamia waandamana kupinga mauaji Kenya
http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2016/07/04/160704083935_kenya_extrajudicial_killings_640x360_bbc.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/mamia-waandamana-kupinga-mauaji-kenya.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/mamia-waandamana-kupinga-mauaji-kenya.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy