WATU watatu walikufa Jumatatu katika kijiji cha Mokubo Kaunti Ndogo ya Kenyenya, Kaunti ya Kisii wakiwa na dalili za kuhara na...
WATU watatu walikufa Jumatatu katika kijiji cha Mokubo Kaunti Ndogo ya Kenyenya, Kaunti ya Kisii wakiwa na dalili za kuhara na kutapika baada ya kula chakula mazishini huku wengine 13 wakikimbizwa hospitalini.
Zaidi ya watu 31 kutoka kijiji cha Nyambunwa,Getacho wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali mbalimbali wakiwa na dalili kama hizo.
Hali hiyo haikuwa nzuri katika maeneo mengine kwa vile familia nyingi walichukuliwa wote hospitali wakionyesha dalili hizo.
Wawili walipoteza maisha yao katika Hospitali ya Royal
mahali walipelekwa kutibiwa,huku mwingine Alvin Mokoro,alikufa katika
hospitali ya kimisheni ya Sengera.
Maafisa wa afya ya Umma katika Kaunti hiyo ndogo
walisema wengi wa wagonjwa hao walikuwa uchovu,kutapika,kuhara kabla ya
kuenda hospitali.
Ndugu yake Alvin Bw George Makori alisema kuwa
marehemu alikuwa na wanakijiji wengine ambao walihudhuria mazishi mawili
alhamisi na Ijumaa kabla ya kuingia nyumbani akihara.
Aliwaeleza kuwa hakula chochote katika mazishi hayo kabla ya kumkimbiza hospitalini mahali ambapo alitangazwa kuwa amefariki.
“Alitueleza hakukula chochote kwenye mazishi hayo kwa hivyo hatujui ni nini ilitendeka,” alisema Bw Makori.
Shangize Bw Makori Bi Jane Bochere na watoto wake
wanne walipelekwa hospitalini kwa sababu walikuwa na dalili za kuumwa na
tumbo kutapika na kuhara huku wakichukuliwa kwenye hospitali ya
kimisheni ya Sengera.
“Wanaendelea kupata matibabu na wanaendelea kupata nafuu,” alisema Bw Makori.
Wanaume 10 na wanawake 7 wamelazwa katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Kenyenya.
Maafisa hao walisema kuwa walishuku ugonjwa wa kuhara na kipindupindu n ahata wakiendelea kusadia maisha ya wakazi.
Bi Agnes Akama, 19, ambaye alikimbizwa katika
hospitali hiyo jumapili asubuhi akiwa anaumwa na tumbo huku akihara
alipatiwa maji na akaambiwa anunue dawa.
Dkt Nyabera Omari msimamizi wa idara afya katika kaunti ndogo hiyo aliambia Taifa wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo.
Alisema wanangoja ripoti kamili kutoka kwa mahabara ambapo walip[eleka sampuli ambayo ilitolewa kutoka kwa wagonjwa hao.
“Tumechukua sampuli mbalimbali za chakula ambayo
walikuwa katika mazishi hayo,damu na kinyeshi chao iliitusaidie kujua ni
ugonjwa gani,” akasema.
Afisa huyo alieleza kuwa tayari wamechukua sampuli za
maji kutoka mto ambao walichota kama umeambukizwa na dalili za
kipindupindu.
chanzo SWAHILIHUB.COM
chanzo SWAHILIHUB.COM