http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Orodha ya Kwanza ya majina ya Wanafunzi waliopata Mikopo Elimu ya Juu 2017/2018


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Dar es Salaam Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema baada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mw...

MARAIS DUNIANI WAVUTIWA NA VITA YA UFISADI TANZANIA
Mwanafunzi askari Chuo cha Anga ajiua
SERIKALI YAINGIZA SUKARI SOKONI


Dar es Salaam
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema baada ya uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018, orodha ya awamu ya kwanza yenye wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo imekamilika.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumatano Oktoba 18,2017 amesema Sh34.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya wanafunzi hao 10,196.

Amesema kwa jumla Sh108.8 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 30,000 wa mwaka wa kwanza kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

Badru amesema orodha ya awamu ya kwanza inapatikana kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo http://www.heslb.go.tz/ na itatumwa kwa vyuo husika.

Amesema orodha nyingine (batches) zitafuata kwa kadri utaratibu wa udahili na uchambuzi unavyokamilika.

“Lengo ni kutoa majina ya wote waliofanikiwa kupata mkopo kabla ya vyuo kufunguliwa mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba, 2017,” amesema.

Mkurugenzi mtendaji huyo amesema orodha hiyo ya wanafunzi 10,196 imepatikana baada ya kupokea na kuchambua awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi 32,495 waliopata udahili katika chuo kimoja.

“Itakumbukwa kuwa moja ya sifa kuu za kupata mkopo ni mwombaji kupata udahili katika taasisi ya elimu ya juu inayotambuliwa na Serikali,” amesema.

Amesema wanafunzi waliopata udahili katika chuo zaidi ya kimoja na ambao wana sifa za kupata mikopo, watapangiwa mikopo baada ya kuchagua na kuthibitisha chuo watakachojiunga kwa ajili ya masomo.

Wakati huohuo, Badru amesema wanatarajia kuanza kutuma vyuoni fedha za mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wamefaulu mitihani yao kuanzia leo Jumatano, Oktoba 18, 2017.

Amesema Sh318.6 bilioni zitatolewa kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo kwa mwaka 2017/2018.

“Tayari Serikali imeshatoa fedha hizo na lengo la Bodi ni kuhakikisha zinafika vyuoni kabla ya kufunguliwa kwa vyuo ili kuwaondolea wanafunzi usumbufu,” amesema.

Bodi imewasihi waombaji wa mikopo kuwa na subira wakati ikiendelea kukamilisha maandalizi ya orodha zinazofuata za wanafunzi waliopata mikopo.

CHANZO: Mwananchi

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Orodha ya Kwanza ya majina ya Wanafunzi waliopata Mikopo Elimu ya Juu 2017/2018
Orodha ya Kwanza ya majina ya Wanafunzi waliopata Mikopo Elimu ya Juu 2017/2018
https://scontent.fdar1-1.fna.fbcdn.net/v/t1.0-9/22490107_1643401562390498_4989392906611906625_n.jpg?oh=2804bc5ba8e04ad320089aeb79c229ea&oe=5A6E0426
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/10/orodha-ya-kwanza-ya-wanafunzi-waliopata.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/10/orodha-ya-kwanza-ya-wanafunzi-waliopata.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy