http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Nassari Awajibu TAKUKURU......"Sitakaa Kimya"


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa hatokaa kimya endapo haoni hatua zinazochukuliwa. Nassari amesema hayo leo Jumanne ...

Majambazi Yavamia Magari ya Mnadani na Kumuua Dereva Mmoja kwa Risasi
SERIKALI INAPANGA WALIMU WA SAYANSI MOJA KWA MOJA BADALA YA KUPITIA HALMASHAURI
Taarifa rasmi ya serikali kuhusu tetemeko la ardhi mkoani Kagera

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa hatokaa kimya endapo haoni hatua zinazochukuliwa.


Nassari amesema hayo leo Jumanne muda mchache baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola kumtaadharisha Nassari kuacha kugeuza taarifa anazoziwasilisha kwenye taasisi hiyo kuwa ni za kisiasa.


Hata hivyo Nassari amesema, “Mlowola inabidi asome sheria ya ‘Whistle blower’ ili nikae kimya lazima nione jitihada zinazofanyika kama hakuna nitaendelea kuongea. Sitokubali kutishwa ili nisiendelee kupeleka ushahidi ninachotaka kuona ni wahusika wanachukuliwa hatua sio madiwani, wahusika wakuu ni mkuu wa wilaya na mkurugenzi,”


Awali akizungumza leo Jumanne asubuhi, Mlowola ametoa tahadhari hiyo kwa Nassari leo Jumanne, Oktoba 17, 2017 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


Amesema endapo Nassari ataendelea kuingiza siasa kwenye suala hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.


Mlowola amesema kitendo cha mwanasiasa huyo kuweka hadharani taarifa za uchunguzi ni kinyume cha sheria kwa kuwa kazi hiyo inatakiwa kufanyika kwa siri na Mahakama ndiyo yenye jukumu la kuchukua hatua.


Amesema Takukuru ina wajibu wa kumlinda mtoa taarifa lakini jukumu hilo linakuwa tofauti kwa Nassari ambaye ameamua kujitokeza hadharani.


"Alicholeta Nassari kwetu ni taarifa si ushahidi. Ameleta tumezipokea na tunazifanyia kazi, inashangaza anapozungumza na vyombo vya habari na kutuelekeza namna ya kufanya kazi," amesema.


Mlowola amesema, "Tulishampa angalizo kuwa mambo tunayoongea ni siri lakini mwenzetu inaonekana anafanya siasa kama anavyosema mwenyewe kuwa ataendelea kuleta ushahidi kama series ya Isidingo."


Mkurugenzi mkuu huyo amemtaka Nassari kuacha kukiingiza chombo hicho kwenye siasa ili kifanye kazi kwa uhuru kama sheria inavyoelekeza.


"Nitoe rai kwa Nassari na wengine wote, ukishaleta taarifa kwenye chombo husika kama hiki kiache kifanye kazi. Hakuna sababu ya kukishinikiza au kukiingiza kwenye malumbano ya kisiasa. Ukweli wa mambo utajulikana mahakamani," amesema.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Nassari Awajibu TAKUKURU......"Sitakaa Kimya"
Nassari Awajibu TAKUKURU......"Sitakaa Kimya"
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiAxZ-dbOLO0e0ciWGBl2iISShDtJOVI17cFAoA7YsSQUcZjjZFVobVCJy7JgO_KeO2OYh5odnrPSaEGJtuLLXJ5X4Bo8pIpg-AfsJJvMZkP3GP9OkSpRhvEk0gxP1ZylItqYh6qI22hUSF/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiAxZ-dbOLO0e0ciWGBl2iISShDtJOVI17cFAoA7YsSQUcZjjZFVobVCJy7JgO_KeO2OYh5odnrPSaEGJtuLLXJ5X4Bo8pIpg-AfsJJvMZkP3GP9OkSpRhvEk0gxP1ZylItqYh6qI22hUSF/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2017/10/nassari-awajibu-takukurusitakaa-kimya.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2017/10/nassari-awajibu-takukurusitakaa-kimya.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy