http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

Mawakili zaidi ya 100 Waandamana kudai haki

MAWAKILI wa kujitegema zaidi ya 100 mkoani Arusha, jana waliandamana kwenda kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, kulaani...

MAWAKILI wa kujitegema zaidi ya 100 mkoani Arusha, jana waliandamana kwenda kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, kulaani kile walichokiita ukandamizwaji wa sheria za nchi na kazi ya uwakili unaofanywa na polisi.

Wanasheria hao wanalaani kitendo cha wakili mwenzao, Shilinde Ngalula, kukamatwa, kufungwa pingu na kufunguliwa mashtaka akiwa kazini Loliondo wilayani Ngorogoro.

Mawakili hao walitembea zaidi ya hatua 400 kabla ya kuzingirwa na polisi ambao waliwataka kuunda kamati ya watu wachache kwenda kuzungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo.

Uamuzi wa kufanya maandamano hayo, ulipitishwa jana mjini hapa baada ya mawakili hao kufanya kikao cha pamoja viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Awali, mawakili hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili Modest Akida, pia walikubaliana kutoendelea na kesi za wateja wao waliokuwa mahakamani.

Akizungumzia maandamano hayo, Akida alisema yalilenga kupinga kitendo cha Jeshi la Polisi wilayani Ngorongoro, kumkamata na kumfungulia mashitaka Wakili Ngalula.

Wakiwa tayari wameandamana umbali wa takribani hatua 400 kutoka mahakamani hapo, vikosi vya askari polisi waliovalia kiraia na wale wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa ndani ya magari mawili, waliwazunguka na kuwaamuru kusimama.

Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Thomas Mareko, aliwataka wanasheria hao kufuata sheria katika kudai na kuwasilisha malalamiko yao.

“Nyinyi ni wanasheria, mpaka hapa tayari mmeshaandamana kinyume cha sheria za nchi, nawaomba chagueni wawakilishi nitawasindikiza mnakokwenda na wengine rudini mkaendelee na majukumu yenu,”alisema Mareko.

Baada ya maandamano hayo kuzuiwa, mawakili hao waliwachagua wawakilishi waliokwenda kuwasilisha malalamiko yao kwa Kamanda Mkumbo na wengine walirudi katika viwanja vya mahakama kusubiri taarifa.

Awali, akizungumza katika viwanja hivyo, Wakili George Njooka alisema mawakili nchini wameanza kudharauliwa na vyombo vya dola.

“Hawa watu walianza na vyombo vya habari, wakaenda kwa wanasiasa na sasa wamekuja kwa mawakili, nawaomba tuanzie hapa twende kwa RPC atuambie haya maelekezo tunayoambiwa yanatoka juu, yanatoka kwa nani,” alisema Wakili Njooka.

Wakili Qamara Peter aliwakumbusha mawakili wenzake kuwa haki siku zote haiombwi bali inadaiwa.

TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

MAGAZETI$type=sticky$count=4


Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mawakili zaidi ya 100 Waandamana kudai haki
Mawakili zaidi ya 100 Waandamana kudai haki
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrBfdEDrYdUWI5taEqx3rLwzIzHAwE778VCLXXtdvktJhLW4BRHG76G5G1-Z8mw5MBjsvi6BpC4rjL3fTPfPIlepZhe8mY_ckKykqvO8wYARpBzF6MeuoVXjtEomaWMts36q0QhtQGuuk/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrBfdEDrYdUWI5taEqx3rLwzIzHAwE778VCLXXtdvktJhLW4BRHG76G5G1-Z8mw5MBjsvi6BpC4rjL3fTPfPIlepZhe8mY_ckKykqvO8wYARpBzF6MeuoVXjtEomaWMts36q0QhtQGuuk/s72-c/1.jpg
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/mawakili-zaidi-ya-100-waandamana-kudai.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/07/mawakili-zaidi-ya-100-waandamana-kudai.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy