Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amehairisha vikao vya bunge leo Mjini Dodoma hadi tarehe 7, mwezi wa 11 saa 3:00 asubuhi ambapo itakuwa sik...
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amehairisha vikao vya bunge leo Mjini Dodoma hadi tarehe 7, mwezi wa 11 saa 3:00 asubuhi ambapo itakuwa siku ya Jumanne.
Waziri Majaliwa ameyazungumza hayo wakati akitoa hoja za Kuhairishwa kwa bunge Mjini humo.
“Mhe. Spika baada ya kusema hayo naomba kusema hoja bunge lako tukufu sasa hadi tarehe 7 siku ya Jumanne mwezi wa 11 mwaka 2017 tutakapo kutana tena hapa saa 3 asubuhi hapa Mjini Dodoma Mhe. Spika naomba kutoa hoja,” amesema Waziri Mkuu.