http://wepesimedia.blogspot.com/p/blog-page.html

post-feature-image

Mbunge Amtaja Kikwete Sakata la EPA


TANGAZA NASISI KWA BEI NAFUU NA UPATE MATOKEO MAZURI KATIKA BIASHARA YAKO.

Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (Cuf), jana aliibua sakata la Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) bungeni akimtaja Rais wa Awamu ya Nne, Jak...

Breki zilivyosababisha vifo 6 na majeruhi 6
Ufafanuzi kutoka Ikulu kuhusu Rais kutengua uteuzi wa Waziri Dr. Kigwangalla
TRC yakitolea maelezo kichwa cha treni kilichopata ajali
Mbunge wa Konde Khatibu Said Haji (Cuf), jana aliibua sakata la Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) bungeni akimtaja Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwamba alikiuka Katiba kwa kutoa msamaha kwa watu waliotuhumiwa.

Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Dk Harrion Mwakyembe ilikanusha madai hayo na kusema Rais alikuwa sahihi kwa kuwa viko vifungu ambavyo vinampa nafasi hiyo.

Katika swali la nyongeza, mbunge huyo alihoji ni kwa nini Kikwete alitoa msamaha kwa watu hao kabla hawajahukumiwa na Mahakama kama Katiba inavyosema.

 “Kama hivyo ndivyo, basi naomba ukubali kuwa Kikwete (Rais mstaafu) alivunja Katiba ya nchi kwa kuwapa msamaha watuhumiwa wa EPA ambao walikuwa hawajahukumiwa bado, naomba majibu,” alihoji Haji.

Katika swali la msingi Mbunge huyo alitaka kujua iwapo Rais kwa mujibu wa Ibara ya 45 (1) A hadi D anayo mamlaka ya kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambao mashauri yake yapo katika vyombo vya dola kwenye hatua za uchunguzi/upelelezi au mahakamani.

Waziri alisema ibara hiyo ni kweli inampa mamlaka Rais ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya Mahakama kupitia kifungu cha kwanza (1).

Dk Mwakyembe alisema kifungu (ii) kinampa Rais Mamlaka ya kumwachia kabisa au kwa muda maalumu mtu yeyote aliyehukumiwa kuadhibiwa kwa kosa lolote.

“Katika kifungu cha (iii) Rais anaweza kubadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu na kifungu cha (iv) anaweza kufuta adhabu yoyote au sehemu ya adhabu,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema kwa kuzingatia masharti ya Katiba, msamaha wa Rais unatolewa kwa mtu aliyetiwa hatiani na kupewa adhabu na Mahakama lakini watuhimiwa wa uhalifu ambao mashauri yao yako hatua za upelelezi au uendeshaji mahakamani hawaguswi na masharti ya ibara hiyo.

Alisema Rais hawezi kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhalifu wa aina yoyote ambao mashauri yao yapo katika vyombo vya dola kwani hatima ya watuhumiwa hao inakuwa bado ipo katika mamlaka za uchunguzi, mashtaka na Mahakama.

Name

BIASHARA NA UCHUMI BREAKING NEWS BURUDANI ENGLISH NEWS GOSIIP GOSPEL HABARI HABARI PICHA MAGAZETI MAKALA MATUKIO MICHEZO MUSIC VIDEO WAZO LANGU
false
ltr
item
WEPESI MEDIA : Mbunge Amtaja Kikwete Sakata la EPA
Mbunge Amtaja Kikwete Sakata la EPA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaaHoGGttc5P0ehnh6zDGnfOzK8VP2PGOy1oUjguc4apnBKhj2pyqsRfd08bobNOc_mNBXnkLtzoDIWG7Wh_Y-ObbfgaXTWTklDvfu0AHuiFjFBx6kw1mj_LACvvbnmCwZiZCUjc_XENYl/s1600/jk.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjaaHoGGttc5P0ehnh6zDGnfOzK8VP2PGOy1oUjguc4apnBKhj2pyqsRfd08bobNOc_mNBXnkLtzoDIWG7Wh_Y-ObbfgaXTWTklDvfu0AHuiFjFBx6kw1mj_LACvvbnmCwZiZCUjc_XENYl/s72-c/jk.png
WEPESI MEDIA
https://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mbunge-amtaja-kikwete-sakata-la-epa.html
https://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/
http://wepesimedia.blogspot.com/2016/05/mbunge-amtaja-kikwete-sakata-la-epa.html
true
925270315725722404
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All

USIPITWE NA HIZI HAPA CHINI LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy