Shirika la Reli Tanzania (TRC), limekanusha kwamba kichwa cha treni kilichopata ajali mwishoni mwa wiki ni miongoni mwa vilivyotelekezw...
Shirika
la Reli Tanzania (TRC), limekanusha kwamba kichwa cha treni kilichopata
ajali mwishoni mwa wiki ni miongoni mwa vilivyotelekezwa bandarini ambavyo vilikutwa havina mwenyewe na Rais Magufuli.
Ofisa
uhusiano wa shirika hilo, Mohammed Mapondela alisema jana kwamba
taarifa hizo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli.
Katika
ajali hiyo, watu 21 walijeruhiwa baada ya treni ya abiria iliyokuwa
ikitokea Tabora kuelekea Kigoma kupata ajali eneo la Malagarasi wilayani
Uvinza.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno alisema
kwamba ajali hiyo ilitokea Februari 27 saa nane mchana.
Katika ajali hiyo, kichwa cha treni kiliacha njia na kuanguka pamoja na mabehewa mawili.
Akifafanua
kuhusu kichwa hicho Mpondela alisema, “Watu wanashindwa kuelewa kuwa
kichwa kilichopata ajali ni 9001 ambavyo ni vya awamu ya kwanza, hivi
vilivyopo bandarini pamoja na kwamba Serikali imeshavinunua bado
havijaanza kutumika.”



