Leo Agosti 14 2017 Baraza la Habari Tanzania chini ya katibu wake mtendaji Kajubi Mkujanga imezunduliwa ripoti ya tukio la uvamizi wa ...

Leo Agosti 14 2017 Baraza la Habari Tanzania chini ya katibu wake mtendaji Kajubi Mkujanga imezunduliwa ripoti ya tukio la uvamizi wa kituo cha Clouds Media Group.
Ripoti hiyo iliyosomwa na Mwanasheria mwandamizi Juma Thomas ambaye ni
Mwenyekiti wa kamati iliyokuwa na watu wanne, imesema Kitendo cha
Makonda kwenda kwenye kituo cha Clouds Media ni kukiuka na kinyume cha
Huduma za vyombo vya habari ambapo ripoti hiyo imeweka wazi kuwa Makonda
aliingilia uhuru wa Vyombo vya habari na Uhariri wa Habari.
Ripoti hiyo inasema Makonda alitafutwa na timu ya uchunguzi bila
mafanikio, na hata walipomwandikia barua hakuna chochote alichojibu,
kwahiyo alijiondolea mwenyewe haki ya kusikilizwa.
TAZAMA FULL VIDEO HAPO CHINI