Debora akiwashukuru watu waliohudhuria sherehe ya kumuaga Na Protte Profit Mmanga KARATU, ARUSHA. Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mah...
Debora akiwashukuru watu waliohudhuria sherehe ya kumuaga
Na Protte Profit Mmanga
KARATU, ARUSHA.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo amemuaga Rasmi Mwanafunzi Debora Laizer, wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Edith Gvora aliyeweka rekodi mkoani Arusha kwa kushinda Nafasi ya kwenda Nchini Malawi kwaajili ya kambi ya Mafunzo ya sayansi kwa wanawake kutokana na mtihani aliofaulu uliotolewa na umoja wa mataifa UN.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, aliyefunga kilemba akiwa na wageni wengine.
Mkuu huyo wa wilaya akimuaga mwanafunzi huyo, amesema ni sifa ya kipekee waliyoipata kama wilaya pamoja na mkoa wa Arusha kupata mtoto wa kike atakayeungana na wenzake tisa toka Tanzania kwenda nchini Malawi kwaajili ya kambi ya sayansi kwa wanawake.
Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kutowafumbia macho watu wanaowapa ujauzito watoto wa kike ili kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua kali za kisheria kuwa funzo kwa wengine.
Debora wa kidato cha tatu ameahidi kufanya vyema katika Kambi hiyo na akiwatoa hofu wasichana wenzake kuwa masomo ya sayansi ni marahisi kujifunza, huku wenzake wakifurahishwa na hatua hiyo na kuahidi kujifunza kwake pindi atakaporejea.

Wanafunzi wakiimba shahiri la kumuaga Mwenzao Debora.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Edith Gvaro, Gidion Myovela, amesema ni furaha kwao kuona mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu kupata fursa hiyo jambo ambalo linawaongezea ari wanafunzi wa kike kupenda masomo ya Sayansi.
Askwar Hilonga ni Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Sayansi cha Nelsoni Mandela, anasema Kambi hiyo itajumuisha wanafunzi wa kike kutoka Nchi mbalimbali, na Tanzania itawakilishwa na Wanafunzi Kumi waliopatikana kwa mchujo mkali nchi nzima sita wakitoka Dar, na watatu Kanda ya Ziwa
Kambi hiyo ya Sayansi kwa wanawake inatarajiwa kufanyika kuanzia July 29, hadi August 13 mwaka huu Nchini Malawi ikifadhiliwa na Ubalozi wa Marekani chini ya Shirika ya Umoja wa Mataifa UN.